Imechapishwa: Mon, Oct 9th, 2017

DYBALA KUPEWA MKATABA WA MAISHA JUVENTUS

TURIN, ITALIA


MKURUGENZI wa klabu ya Juventus, Giuseppe Marotta, ameweka wazi kuwa wapo kwenye mipango ya kutaka kumpa mkataba wa maisha mshambuliaji wao, Paulo Dybala.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye yupo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina, mapema Aprili mwaka huu aliongeza mkataba wa miaka mitano ndani ya kikosi hicho na kumfanya achukue kitita cha pauni 110,000 kwa wiki.

Klabu kubwa barani Ulaya kama vile Barcelona, Real Madrid, Manchester United zilikuwa zinawania saini ya mchezaji huyo, lakini Juventus wamejipanga kuhakikisha mchezaji huyo anaendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa maisha yake kwa kumpa ofa nono.

“Hatuna mpango wa kumuuza Dybala, tunaheshimu mchango wake ndani ya klabu hii hasa kutokana na umri wake, hivyo klabu hii ina mipango mirefu na mchezaji huyo.

“Mchezaji mwenyewe amefanya mazungumzo na uongozi na amekubali kuwa hapa kwa maisha yake yote, tunaamini maamuzi hayo yapo kwenye kichwa chake, lakini lengo letu ni kuhakikisha tunaweka ofa nyingine nono ili kumfanya aendelee kuwa hapa, tunaamini yupo tayari kusaini mkataba huo hivi karibuni,” alisema Moratta.

Dybala hadi sasa amefanikiwa kupachika mabao 10 katika michezo saba ya Ligi Kuu nchini Italia msimu huu, hivyo amekuwa mchezaji ambaye anategemewa kwa kiasi kikubwa katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

Hata hivyo, ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina katika michuano ya kuwania kufuzu Kombe la dunia 2018 nchini Urusi, wiki hii wanashuka dimbani katika mchezo wa mwisho dhidi ya Ecuador, watahakikisha wanashinda mchezo huo ili kujihakikishia wanashiriki Kombe la dunia mwakani, lakini wakiupoteza safari yao itakuwa imefikia mwisho.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

DYBALA KUPEWA MKATABA WA MAISHA JUVENTUS