23 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dunia yalaani kifo cha Khashoggi

ISTANBUL, UTURUKI

MAELFU ya watu duniani wanaofuatilia mkasa wa kuuawa mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi, katika ubalozi wa Saudi Arabia nchini Uturuki, wamelaani vikali tukio hilo ambalo limetajwa kuwa pigo katika haki za binadamu pamoja na usalama.

Wakati dunia ikilaani tukio hilo, mtoto wa kiume wa mwandishi huyo aitwaye Salah Khashoggi, amewasili mjini Istanbul akiwa njiani kuelekea nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani, nchi hiyo inakaribisha uamuzi wa Saudi Arabia wa kumwachia kijana huyo atoke nchini humo.

Hapo awali shirika linalopigania haki za binadamu Human Rights Watch lilisema Salah Khashoggi na familia yake wanaelekea Marekani baada ya kuondolewa vikwazo vya kusafiri.

Katika hatua nyingine, maelfu ya waombolezaji pamoja na maandamano makubwa yanaendelea mjini Istanbul kudai waliomuua Khashoggi wafikishwe mahakamani.

Mtafiti wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa, Agnes Callamard, amewaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya jumuiya hiyo ya kimataifa kuwa mauaji ya Khashoggi yamepangwa makusudi na waliomuua ni maofisa wa ngazi ya juu wanaoweza kuiwakilisha Serikali ya nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles