23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dubai yadaiwa kuficha mafisadi, watakatishaji fedha

BERLIN, UJERUMANI

SHIRIKA la Kimataifa la Kupambana na Ufisadi la Transparency International limesema jiji la Dubai huko nchini Falme za Kiarabu (UAE), limekuwa maficho salama ya watakatishaji wa fedha chafu duniani kiasi kwamba mafisadi na wahalifu wengine wanaweza kununua majumba ya kifahari katika eneo hilo bila kizuizi chochote kutoka mamlaka za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Transparency International, matokeo ya uchunguzi wa jumuiya kadhaa za kimataifa yanaonesha kwamba, jiji la Dubai ni maficho ya wahalifu wanaotakatisha fedha.

Taarifa hiyo inaonyesha kwa mara nyingine Transparency International ikilitaja jiji la Dubai kama maficho ya wahalifu wa kimataifa.

Wakati Shirika hilo likibainisha hali hiyo, siku chache zilizopita pia Jarida la kibiashara na uchumi la Forbes la nchini Marekani liliandika kuwa licha ya sura hasi inayofungamanishwa na Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusiana na utakatishaji wa fedha chafu, serikali ya nchi hiyo haijachukua hatua za maana za kukabiliana na uhalifu huo.

Juni mwaka jana pia gazeti la The Guardian la Uingereza liliripoti kuwa, jiji la Dubai limekizidi kisiwa cha Puerto del Carmen kilichoko kusini mwa Hispania, ambacho ni maarufu kuwa ndilo eneo baya zaidi duniani kwa utakatishaji wa fedha chafu na haramu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles