26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DPP alia faulo kesi za udhalilishaji Pemba

Na KHAMIS SHARIF

ZANZIBAR

OFISI ya Mkurugenzi wa Mashtaka Kisiwani Pemba, imesema bado wananchi wana uwelewa mdogo wa kupinga udhalilishaji.

Imesema  baaadhi ya wananchi  huwasilisha barua   katika ofisi hiyo za madai ya kuomba kufutwa  kesi za jinai zikiwamo za udhaliliushaji.

Mwanasheria wa Ofisi ya DPP, Ali Rajab Ali, alikuwa akizungumza na MTANZANIA hivi karibuni kwenye maonyesho ya Siku ya Sheria.

Alisema hatua hiyo imekuwa ikiwashangaza hasa kwa jamii kushindwa kuona umuhimu wa mashauri hayo kama yanalinda haki za watu badala ya kutaka kesi zifutwe.

“Kila mwezi tumekuwa tukipokea kati ya maombi 15 hadi 20  kutoka kwa wananchi wakiomba kufutwa   kesi zao zikiwamo za udhalilishaji, jambo ambalo huwa linatupa mshangao.

“Baada ya mwananchi kupatwa na masahibu ya kesi za udhalilishaji sisi wakati wote tupo tayari kuona kesi inakwenda mbele lakini baada ya muda huletwa barua za kuomba kufutwa  kesi hizo.

“Tena kinachoumiza zaidi ni kesi hizo zipo zile zinazolalamikiwa sana na jamii zikiwamo za udhalilishaji lakini ikifika mahakamani kwa ajili ya ushahidi huwa ngumu,” alisema Ali.

Mwanasheria huyo alisema miongoni mwa sababu ambazo huandikwa na wananchi hao  ni kwa mtuhumiwa kufunga ndoa na muathirika wa tukio.

Akizungumzia sababu za nyingine kutaka kufutwa   kesi hizo, Ali alisema, ni   undugu baina ya mtuhumiwa na aliyefanyiwa kitendo cha udhalilishaji.

“Huwa tunakaa nao nje ya mahakama na kuwaeleza kuwa sheria zetu zinakataza kufutwa   kesi yoyote ya jinai, na kuwaomba wafike mahakamani kutoa ushahidi na wapo wanaotii hilo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles