31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DPP aiomba mahakama itupilie mbali rufaa ya kina Mbowe, Matiko

KULWA MZEE

MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP) ameomba Mahakama ya  Rufaa iamuru rufaa iliyofunguliwa Mahakama Kuu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakipinga kufutiwa dhamana itupiliwe mbali na kwamba rufaa hiyo ni batili.

Akiiwakilisha Jamhuri mbele ya jopo la majaji watatu, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amedai wajibu maombi waliwasilisha rufaa Mahakama Kuu mbele ya Jaji Sam Rumanyika bila kuambatanisha uamuzi wa Mahakama ya Kisutu na mwenendo wa kesi hiyo.

Nchimbi alidai rufaa yao ina sababu tatu ambapo sababu ya pili inayodai kwamba Jaji Rumanyika alikuwa  na upendeleo aliiondoa baada ya jopo kuhoji na kuonekana haijawahi kuwasilishwa Mahakama Kuu.

Jopo la majaji hao, Stellah Mugasha, DK. Gerald Ndika na Mwanaisha Kualiko.

Nchimbi anadai kwa kupokelewa kwa rufaa ya kina Mbowe Mahakama Kuu ikiwa hakijaambatanishwa na uamuzi na mwenendo wa kesi kama Sheria namba 362(1) inavyoelekeza kunaifanya rufaa hiyo kuwa batili na kuonekana haiko sahihi mahakamani.

Akijibu Wakili Peter Kibatala alidai rufaa hiyo iliwasilishwa mahakamani bila sababu za msingi na kwamba hakuna ubishi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu hakuwa na mamlaka ya kuita jalada la kesi na kuendelea kusikiliza rufaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles