DONDOO

0
854


Chelsea

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard, ameweka wazi kuwa ataondoka ndani ya klabu hiyo mwakani endapo watashindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Real Madrid.

AC Milan

UONGOZI wa klabu ya AC Milan upo kwenye mipango ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Paris Saint-Germain, Adrien Rabiot, wakati wa uhamisho wa dirisha dogo Januari. Mchezaji huyo anatarajia kumaliza mkataba wake msimu wa 2018-19.

Real Madrid

MATAJIRI wa soka nchini Hispania, Real Madrid, wameanza kumuwinda kinda wa Manchester City, Brahim Diaz. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na amedai hataki kuondoka kwa mkopo.

Napoli

UONGOZI wa klabu ya Napoli, umethibitisha kuwa unakaribia kumalizana na beki wao wa pembeni, Elseid Hysaj, kwa ajili ya kumpa mkataba mpya. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akiwindwa na klabu ya Juventus.

Man United

MIPANGO ya Manchester United ni kuhakikisha inamwongezea mkataba mpya nyota wake, Ander Herrera, ili aweze kubaki kwenye viwanja vya Old Trafford. Mkataba wa mchezaji huyo unatarajia kumalizika majira ya joto mwakani.

Juventus

MATAJIRI wa soka nchini Italia, Juventus, wameingia kwenye vita dhidi ya Inter Milan kwa ajili ya kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Fiorentina, Federico Chiesa. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, tayari ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia.

Tottenham

KINDA wa klabu ya Ajax, Frenkie De Jong, anaweza kuonekana akiwa na uzi wa klabu ya Tottenham katika kipindi cha Januari mwakani kutokana na klabu hiyo kuonesha nia ya kuitaka saini yake. Hata hivyo, Tottenham haijafanya usajili wakati huu wa kiangazi.

Man United

KOCHA wa klabu ya Wolves, Nuno Espirito Santo, ametajwa kwenye orodha ya makocha wanaowindwa na klabu ya Manchester United kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Jose Mourinho endapo atafungashiwa virago vyake.

Barcelona

KIUNGO wa klabu ya Barcelona, Sergio Busquets, anatarajia kukutana na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kusaini mkataba mpya. Mazungumzo ya mkataba mpya yalianza kuzungumzwa tangu mapema mwaka huu na sasa wamefikia hatua za mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here