26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DOGO JANJA: WANAUME NI WAONGO SANA

NA JESSCA NANGAWE


MSANII wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chande maarufu kama Dogo Janja, amefunguka na kuwapa ushauri wanawake kuwa wawe makini na maisha na si kuwategemea wapenzi wao kwa kuwa wanaume ni waongo sana.

Dogo Janja ambaye ni mume wa msanii wa filamu, Irene Uwoya, amesema ni vyema wanawake wengi wakajiongeza na kujitegemea kwa kufanya shughuli za kujiingizia kipato au kuhakikisha anajituma ili aweze kuyamudu maisha kwa ujumla.

“Wanawake watambue kuwa anayekupa hela ya kula na anayekupa kazi upate hela ya kula ni bora anayekupa kazi, huyo mwingine hakutakii mema zaidi ya kukuharibia maisha yako ya baadaye,” alisema Dogo Janja.

Alisema anafurahi kuona wanawake wengi wakijipatia fursa za kuendeleza maisha yao hali inayowafanya kujitofautisha na maisha ya zamani ambayo wengi walikua wanashindwa kutumia fursa wanazokutana nazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles