24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DODOMA FC YAKABIDHWA RC

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, amemkabidhi timu ya Dodoma FC Mkuu mpya wa Mkoa huo, Dk. Benelith Mahenge.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli, alifanya mabadiliko kwa wakuu wa mkoa ambapo Rugimbana aliondolewa na Dk. Mahenge akibadilishwa kutoka mkoani Ruvuma na kwenda Dodoma.

Dodoma FC inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ambapo mpaka  mzunguko wa kwanza ulipomalizika juzi timu hiyo  inaongoza kundi C kwa  kujikusanyia  pointi 18.

Akizungumza juzi mjini hapa wakati wa makabidhiano ya ofisi, Rugimbana alisema anaondoka Dodoma lakini mojawapo ya majukumu anayomwachia Dk. Mahenge ni kuhakikisha Dodoma FC inapanda  ligi kuu.
Rugimbana alisema makao makuu ya nchi yameshahamia Dodoma, hivyo ni lazima kuwe na timu ya ligi kuu.

Alisema timu ya Dodoma FC inashiriki Ligi Daraja la Kwanza, hivyo ni lazima aipe ushirikiano wa hali na mali ili iweze kufanya vizuri katika ligi hiyo.
 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles