30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DK. TIZEBA ‘ATUMBUA’ VIGOGO WATATU

Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba amewatumbua maofisa watatu wa Idara ya Maendeleo ya Mazao, kitengo cha pembejeo mkoani Geita, akiwamo Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo hicho, Shenal Nyoni Ofisa Kilimo Daraja la kwanza, Michael Mayabu wa mkoani Geita, kwa kujaribu kuiibia serikali kupitia vocha za pembejeo za zaidi ya Sh bilioni 26.

Maofisa hao wanadaiwa kushirikiana na mawakala wa pembejeo kuchezea mfumo wa taarifa za pembejeo na kuchapisha zenye thamani ya fedha hizo na kuzipeleka kwa wakulima pamoja na zile zilizochapwa kihalali za Sh milioni 38.

Dk. Tizeba amesema leo kuwa hatua hiyo pia imetokana na ukosefu wa umakini na usimamizi mzuri wa sheria ya ununuzi wa umma ikiwamo kusababisha kuchapishwa kwa vocha za pembejeo zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 78.5 ambazo ni zaidi ya bajeti halisi iliyotengwa kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo kwa kiasi cha Sh bilioni  42.5.

“Tumepitia taarifa ya waraka wa mkakati wa utekelezaji na usimamizi wa utoaji wa ruzuku za pembejeo za kilimo kwa wakulima kwa kutumia mfumo wa vocha wa mwaka 2015/2016, wakati wa utekelezaji wa zoezi la usimamizi wa mpango huu

msimu wa mwaka 2014/2015 – 2015/2016 kulijitokeza tuhuma mbalimbali zilizohusu ukiukwaji wa taratibu uliofanywa na watumishi wa serikali za mitaa zilizohusika kwenye Mpango wa Ruzuku.

“Watumishi hao walituhumiwa kushirikiana na mawakala waliokuwa wamepewa dhamana ya kusambaza pembejeo katika kuhujumu mpango huo serikalini ambapo Wizara ya Kilimo ilichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwasimamisha kazi watumishi watano wa Idara ya Maendeleo ya Mazao, Sehemu ya Pembejeo waliohusika kusimamia mpango wa Ruzuku za Pembejeo za kilimo,” amesema Dk. Tizeba.

Dk. Tizeba amesema kutokana na hali hiyo, zaidi ya Sh bilioni 29.9 zingepotea kama kusingekuwa na umakini katika uhakiki kwani katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 serikali ilitenga Sh bilioni 35.4 kwa ajili ya pembejeo za kilimo na mara baada ya zoezi la utoaji ruzuku ilibainika kuwa deni lililowasilishwa serikalini na mawakala ilikuwa ni Sh bilioni 65.4.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles