24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Shein atoa maagizo Wizara ya Kilimo Zanzibar

Mwandishi wetu – Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameitaka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kuhakikisha miche ya karafuu inayotolewa na Serikali kwa wakulima, inakuwa imekomaa ili kuondokana na uwezekano wa kufa inapooteshwa mashambani.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zanzibar jana, ilisema Dk. Shein alisema hatua hiyo itaondoa malalamiko kutoka kwa wakulima wa zao hilo kuwa miche mingi hufa baada ya muda mfupi wa kupandikizwa, kwa vile haikuwa katika kiwango bora cha kukomaa.

Alisema ni muhimu kwa watendaji wanaoshughulikia ugawaji wa miche hiyo kuhakikisha inawafikia walengwa wa kilimo hicho, ili kuondokana na manung’uniko kwa baadhi ya wakulima kukosa miche hiyo.

Aidha, Dk. Shein aliwataka wananchi wenye taarifa za mashamba yenye mkanganyiko, kutoa taarifa serikalini ili ziweze kutathminiwa.

Naye, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri alisema ukodishwaji wa mashamba ya mikarafuu katika eka za Serikali hufanyika kupitia kamati maalum, ambapo ugavi wa fedha zinazopatikana hugawiwa kati ya Serikali na mhudumiaji kuambatana na mazingira ya shamba linavyoshughulikiwa na kuendelezwa.

Mjawiri alisema Serikali inaendelea na mchakato wa kuyaandalia hati miliki mashamba yote ambayo hadi sasa hayajatambuliwa, ili wananchi wanaoyatunza waweze kuyaendeleza.

 Alisema Serikali huyachukuwa mashamba hayo ya mikarafuu baada ya kujiridhisha kuwa ni eka za Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles