24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘Dk. Shein ajiuzulu urais Zanzibar’

Dr.-Ali-Mohamed-SheinNa Waandishi Wetu, Dar es Salaam

ALIYEKUWA Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud, amesema hakuna namna ya kutatua mgogoro wa siasa unaoendelea ila ni kuifuata Katiba ya Zanzibar inayoruhusu Rais kujiuzulu na madaraka yake kuchukuliwa na Jaji Mkuu.

Hayo aliyasema   Dar es Salaam jana alipowasilisha mada kwenye kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS).

“Hakuna namna ya kutoka katika mkwamo huu isipokuwa kurudi kwenye Katiba ya Zanzibar,” alisema Masoud.Alisema kwa mujibu wa Katiba hiyo  Ibara ya 34(1)(i) Jaji mkuu anaweza kuchukua madaraka ya Rais  atakapojiuzulu.

Kwa sababu hiyo alimtaka  Dk. Ali Mohamed Shein, ajiuzulu ili Jaji Mkuu ashike madaraka ya rais na aunde Tume huru ya kuchunguza suala  la kufutwa  uchaguzi.

Alisema endapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Salum Jecha, atapatikana na makosa kwa kitendo alichofanya achukuliwe hatua za sheria.

Katika kongamano hilo lililokuwa na mada iliyosema ‘Changamoto za Kisheria zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’,  Masoud alieleza jinsi  Jecha alivyokiuka sheria kwa kuamua kufuta uchaguzi huo.

Alisema Jecha alifuta uchaguzi kwa kushauriwa na watu suala ambalo ni kinyume cha sheria ya uchaguzi inayokataza tume kuingiliwa katika uamuzi.

“Jecha mwenyewe alisema alikaa na vyombo vya dola kabla ya kufuta uchaguzi na wala si kikao cha ZEC hivyo haukua uamuzi wa Tume,” alisema Masoud na kuongeza: “Ukiukaji wa sheria alioufanya Jecha hauna mfano wa kufananishwa nao kwani ni wa hali ya juu”.

Alisema mkwamo uliotokea Zanzibar si Jecha wala Tume wa kulaumiwa kwa sababu  si uamuzi wao bali kuna jambo lililojificha ambalo litakuwa   hatari kwa Taifa.

“Kuna kitu hatuambiwi wala hatukijui na kinaweza kuwa hatari endapo serikali itaendelea kufanya mambo yao hivi,” alisema Masoud.

Mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, Fatma Karume, akiwasilisha mada yake alisema kuna upungufu mkubwa wa katiba na sheria ambazo zinampa mamlaka makubwa rais.

“Rais ana mamlaka ya kumchagua Mwenyekiti wa Tume tena kwa kuzingatia sifa zilizopo kwenye Katiba ambazo ni kuwa na sifa ya kuwa Wakili wa Mahakama Kuu au anayeheshimika kwenye jamii,” alisema Fatma.

Alisema sifa aliyonayo Jecha ni ya kuheshimika ambayo hata hivyo imehojiwa endapo ana sifa hiyo tena baada ya kufuta uchaguzi.Rais anatakiwa asiruhusiwe kuchagua majaji kwa vile linapokuja suala linalomgusa si rahisi kwa majaji kutenda haki, alisema.

“Huu mgogoro uliopo ilitakiwa wanasheria tuwe bize tunakimbizana kwenda kufungua kesi lakini tupo kimya kwa sababu huyo aliyewachagua majaji ndiye aliyemchagua Jecha,” alisema Fatma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles