23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Shein aandaa chakula kwa vijana wa halaiki

Mwandishi Wetu – Mjini Mgharibi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameungana pamoja na Vijana wa Halaiki na wahamasishaji  walioshiriki katika maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika chakula maalum alichowaandalia.

Chakula hicho maalum cha mchana aliwaandalia  kinatokana na ushiriki wao kwenye sherehe hizo za miaka 56, zilizofanyika January, 12 mwaka huu katika Uwanja wa Amani,mjini Unguja.

Hafla  hiyo ilifanyika jana katika viwanja vya Polisi Ziwani na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwemo Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma.

Wengine ni pamoja na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Mawaziri, Naibu Mawaziri pamoja na Washauri wa Rais wa Zanzibar.

Katika shukrani zake Rais Dk. Shein kwa vijana hao zilizotolewa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi, Issa Haji Ussi ‘Gavu’, alisema ana imani kubwa kuwa vijana hao watakuwa sehemu ya ulinzi wa Taifa hili kutokana na kujitowa kwao na uzalendo waliouonesha.

Alisema katika kipindi chote cha maandalizi ya sherehe hizo  vijana hao  walikuwa wakipokea vyema maelekezo wanayopewa na Viongozi wao  na kuyafanyia kazi kwa maslahi ya taifa.

Aliwatakiwa kheri na mafanikio katika masomo yao ili waweze kufaidika katika maisha yao na kulisaidia Taifa kupiga hatua za kimaendeleo. 

Aidha, alimpongeza Rais Dk. Shein kwa uongozi wake madhubuti uliopelekea kuwepo kwa amani na utulivu, umoja  na mshikamano, na kusema  umesaidia sana kuharakisha maendeleo ya kiuchumi hapa nchini.

Naye, Katibu wa Halaiki na Uhamasishaji,  Ali Mohamed Baraka alitoa shukurani za dhati kwa Rias Dk. Shein kwa mwaliko huo na kutoa ahadi ya vijana hao kuendelea kushirikiana na Serikali ili kufanikisha  vyema  shughuli  zinazoandaliwa.

Aidha, alimshukuru Rais Dk. Shein kwa kuwa karibu na vijana hao na kuonyesha imani upendo mkubwa kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles