27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. MWANJELWA AONYA RUSHWA MPAKA WA HOLILI

Na Kamili Mmbando, Aliyekuwa Kilimanjaro.


SERIKALI imesema itawachukulia hatua za kisheria watumishi wanaojihusisha na rushwa kwenye mpaka wa Holili unaotenganisha Tanzania na Kenya.

Hayo yalisemwa juzi mkoani Kilimanjaro na Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa, alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi, ambapo alikemea vitendo vya baadhi ya watumishi wasio waaminifu kwenye mpaka wa Holili.

“Serikali itawachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo vya rushwa mpakani na kukwamisha wafanyabiashara washindwe kusafirisha bidhaa zao.

“Wafanyakazi wanaofanya biashara kwenye mpaka wa Holili wanalalamikiwa sana na wafanyabiashara wa mazao kuwa wamekuwa wakiwaomba rushwa, japo wanakuwa wamefuta taratibu zote za usafirishwaji wa mazao nje ya nchi,” alisema.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agness Hokororo, alisema mpaka wa Holili una changamoto kubwa hasa za uwepo wa njia za panya zipatazo 100 ambazo hutumika katika kuvusha mazao ya bishara kinyume cha sheria.

“Moja ya changamoto ni kuwepo na njia za kusafirishiwa mazao zisizo rasmi nyingi, jambo ambalo linatufanya tujitahidi kuongeza ulinzi kwani  changamoto bado ni kubwa,” alisema Hokororo.

Pamoja na hali hiyo, Dk. Mwanjelwa alitembelea mpaka huo upande wa Kenya kuona namna usafirishwaji wa mazao unavyofanywa na baadaye kuelekea Namanga mkoani Arusha ambako nako alitembelea eneo la Tanzania na kuwapongeza watumishi wa mkapa huo kwa kufanya kazi nzuri, ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato ambayo yamevuka kiwango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles