25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DK. MPANGO: SITISHWI NA MAKONDA

Na Benny Mwaipaja-WFM, Dar es Salaam


WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ameagiza kupigwa mnada kwa makontena 20 yaliyoingizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amesema katu haogopi vitisho vya Makonda kwani kodi inayodaiwa baada ya kuingizwa kwa makontena hayo inatakiwa kulipwa kwa mujibu wa sheria.

Kauli hiyo aliitoa jana Dar es Salaam baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo yalipohifadhiwa makontena hayo katika Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD).

Aliiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia Sh bilioni 1.2.

Dk. Mpango, alisema kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na mkuu huyo wa mkoa, vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini, akitumia vifungu vya Biblia, kwamba yeyote atakayenunua mzigo huo atalaaniwa.

““Yapo mambo yanasemwasemwa kwenye vyombo vya habari, video clips, kwenye magazeti, sisi tunachofanya ni kusimamia matakwa ya sheria za nchi na sio vinginevyo.

“Na Sheria za nchi hazichagui sura wala cheo cha mtu, na mimi ndiyo nilichoapa. Niliapa kutekeleza sheria za nchi kwanza, nililotaka kusema kamishna katika suala la kusimamia sheria za kodi ya forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, sheria zetu za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kadhalika, simamia sheria bila kuyumba,” alisisitiza Dk. Mpango wakati akitoa maelekezo kwa Kamishna wa Forodha, Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba aliyeagiza (Makonda) alipe kodi stahiki na asipolipa, mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Wakatiumefika sasa kwa viongozi wa serikali kutumia vikao husika kujadiliana masuala ya utawala au haya yenye utata ya makontena badala ya kutumia majukwaa ya umma, media kujadili masuala tata na kuumbuana. Kutoa matamko hadharani ipigwe marufuku mpaka kikao cha mjadala kisanyike kisiri na maamuzi yafikiwe halafu umma uarifiwe. Inapofika maamuzi ya kiongozi kutaka kufanya ukaguzi wa kushitukiza-asitangaze na akifanya asiongozane na media ya umma isipokuwa Afisa habari ya Wizara yake. Akisha kukagua na kupata taarifa ndio anaweza kuita media na kutoa ktk umma.Tumia vikao kuongea na unakopekua kabla ya matangazo. Eti nitavamia-wanajiandaa kuficha maovu hata watu na kupika taarifa. Anayevamiwa haarifiwi.Makosa mengi yanakuwa ya Serikali hivyo inavunja imani yake kwa wannanchi. Uchimbaji madini utafanyikaje katika makazi ya watu bila wizara ya madini na NEMC kujua. Wageni wataingiaje nchini kufanyakazi miaka bila hati ya ruhusa na Wizara inatakiwa kukagua viwanda, uwekezaji na pia masuala ya OSHA kwa wafanyakazi. Wanaofanyakazi za kuzoa taka na kufagia barabara wanaonekana mijini na viongozi husika wanaona hawana protective gear. uuzaji vyakula wazi barabarani upo mpaka nje ya majengo ya mawizara na barabara kuu wapitazo viongozi. feeder roads na footpaths zimezibwa na wafanyabiashara na majengo yapo ktk wetlands, ambwawa ya kinyesi na majalala ya taka ngumu. Yamewekewa namba za serikali za mitaa, maji ya Dawasa na umeme wa Tanesco-nani haoni kuwa haya makosa. Garage na karakana za magari katika wetlands na zina vibali. Magari yanaoshwa mabarabarani yanamwaga maji meusi ya lead mji mijini na karakana za kutengeneza magari kando ya barabara kuu na maji machafu ya kuosha magari yanazagaa.Nani haoni. kaeni vikao vya management vya mawizara myajadili na kuchukua hatua badala ya kuumbuana ktk media. Inatuchosha wananchi kuona kila sekta ina utata usio tatuliwa ila viongozi kuumbuana hadharani daily badala ya kupanga mipango ya utatuzi ikatekelezwa efficiently and effectively na TOR zipo ila kila mtu akiongea ni kusema-kama alivyoagiza Rais wa 5 Mheshimiwa…..! Ina maana huna TOR? Hujui wajibu wako?! Hufanyi mpaka kiongozi akuambie? Mbona sera na sheria na mikakati mingine ni toka tupate uhuru inaboreshwa tu lakini ni yale yale hatufanyi? Tujirekebishe ili tufikie ufanisi unaotajiwa kwa joint work.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles