27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DK. KIGWANGALLA: TUMIENI TEKNOLOJIA YA SIMU KUZUIA UHALIFU

Na LILIAN JUSTICE-MOROGORO

NAIBU Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla, amekitaka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kitumie tafiti zake za teknolojia ya simu, kukabiliana na uhalifu.

Dk. Kigwangalla aliyasema hayo juzi wakati alipotembelea banda la SUA lililoko katika viwanja vya maonyesho ya wakulima Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mjini Morogoro.

“Teknolojia ya kuzuia uhalifu inayofanywa na SUA inapaswa kuendelezwa zaidi ili iweze kusambazwa kwa wananchi wote nchini ili iweze kuwa na faida.

“Teknolojia hiyo isipofikishwa kwa wananchi ili waweze kuitumia, haitakuwa na maana yoyote kwani lengo ni mwananchi kuweza kunufaika na tafiti mbalimbali zinazozalishwa na wataalamu wetu nchini,” alisema Dk. Kigwangalla.

Awali, akielezea kuhusu teknolojia hiyo, mhandisi Algen Denis wa Idara ya Sayansi na Uhandisi chuoni hapo, alisema telnolojia hiyo inaweza kufungwa majumbani ama sehemu za vituo vya biashara ili mhalifu anapofika kwa lengo la kujaribu kuiba, mlio maalumu unatokea ili kuashiria kuna wizi unaotaka kufanyika eneo husika.

“Teknolojia hiyo ambayo huzalishwa SUA katika idara ya uhandisi, inauzwa kwa shilingi 500,000 ili wananchi wengi waweze kuitumia kwa ajili ya usalama wa mali zao.

“Pamoja na hayo, nawaomba wananchi wafike chuoni kwetu ili wajifunze teknolojia hiyo inayozalishwa ili waweze kuitumia vema katika suala la kuzuia uhalifu kwa njia ya simu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles