23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DK. KALEMANI AZINDUA REA III RUKWA

Na MWANDISHI WETU

-RUKWA

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani, amezindua Mradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA PHASE III) katika Kijiji cha Kabwe, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa.

Akizungumza katika uzinduzi huo jana wilayani hapa, Dk. Kalemani alisema jumla ya Sh bilioni 42.5 zitatumika kupeleka umeme katika mkoa huo, ambako mradi huo utatekelezwa katika vipindi viwili tofauti. Sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 111.

“Sehemu ya pili itahusisha vijiji 145, ambayo itaanza baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza. Kufikia mwaka 2021 vijiji vyote vya Mkoa wa Rukwa vitakuwa vimepatiwa umeme,” alisema Dk. Kalemani.

Katika uzinduzi huo, Dk. Kalemani alimtambulisha Mkandarasi atakayejenga Mradi wa REA III mkoani humo kuwa ni Kampuni ya Nakuroi Investment Company Limited ya hapa nchini.

Alimwagiza Mkandarasi kuhakikisha anapeleka umeme kijiji kwakijiji na kitongoji kwa kitongoji bila kuruka na sehemu zinazotoa huduma za kijamii kama shule, zahanati, magereza, visima vya maji, nyumba za ibada na sehemu mbalimbali.

Pamoja na hali hiyo, aliitaka Tanesco kufungua ofisi katika Kijiji cha Kabwe na maeneo yote yenye wateja wengi, lakini wapo mbali na huduma za Shirika hilo la Umeme.

Awali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tanesco, Dk. Tito Mwinuka, aliwaomba wananchi wa Kabwe kuwa waaminifu na kutoa ushirikiano kwa watendaji wa Tanesco kabla na hata baada ya mradi kukamilika.

“Muitunze miundombinu ya umeme, msiihujumu wala kuichoma moto,” alisema Dk. Mwinuka.

Alisema TANESCO imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme iliyobora na ya uhakika.

Naye Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy (CCM), alisema mradi huo wa usambazaji umeme vijijini hauna malipo ya fidia, hivyo watoe ushirikiano kwa wakandarasi hao wakati wanatekeleza mradi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles