31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DK. KALEMANI AISHUKURU SERIKALI UJENZI HOSPITALI YA RUFAA CHATO

Mbunge wa Chato, Dk. Medard Kalemani, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, akimtambulisha kwa kina mama walioepeka watoto wao Kliniki leo, katika Hospitali Wilaya ya Chato, ambapo alitumia fursa hiyo kumtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile

Na BAKARI KIMWANGA-CHATO       |


Mbunge wa Chato, Dk. Medard Kalemani (CCM), ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vya afya wilayani Chato.

Hospitali hiyo kubwa ya kisasa inajengwa na serikali kwa gharama ya Sh bilioni 9.1 ambapo hadi sasa zimetolewa Sh bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi huo.

Dk. Klemani ambaye pia ni Waziri wa Nishati, amesema ujenzi wa hospitali hiyo itasaidia wananchi wa mikoa ya Geita na Kagera ambao walikuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma za afya kwa madaktari bingwa.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake ya kibunge kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, leo Mjini Chato, alisema kuwa anaishukuru Serikali wakati wote kwa kusaidia maendeleo ya jimbo lake hasa kwenye sekta ya afya.

“Ninaishukuru Serikali pamoja na nawe Mheshimiwa Naibu Waziri ambaye muda wote umekuwa msaada kwetu wananchi wa Chato, kwa miaka mitatu mfululizo ninapoleta maombi yangu ya ujenzi wa vituo vya afya muda wote wizara yako imekuwa ikitupa fedha.

“Na kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Chato, itakuwa mkombozi kwani itaweza kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa Chato, Geita, Muleba na Biharamulo.

“Hata hivyo bado ninaishukuru sana Serikali kwa mwaka wa tatu mfululizo niliomba pesa kwa ajili ya zaidi ya Shilingi milioni 400 ujenzi wa kituo cha afya Bwanga nilipewa. Na bado hata Chato tuliletewa magari mawili ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ambayo ni mazima na yanatoa huduma nzuri,” amesema Dk. Kalemani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles