24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

DK JONAS BENEDICT KUMRITHI MANJI

NA ZAITUNI KIBWANA
Siku moja baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kutangaza kwamba uchaguzi wa klabu ya Yanga upo pale pale, Dk Jonas Benedict amejitokeza na kuchukua fomu kurithi nafasi ya Yusuph Manji.

Akizungumza na Bingwa, Wakili Ally Mchungahela amesema Dk Benedict ni mgombea pekee wa nafasi ya mwenyekiti aliyejitokeza mpaka sasa kuchukua fomu hiyo.
Amesema kigogo wa zamani wa klabu hiyo, Yona Kevela naye amechukua fomu kutaka nafasi ya makamu mwenyekiti katika uchaguzi huo.

Wakili huyo amesema wajumbe tisa waliojitokeza hadi sasa ni Dominic Francis, Pindu Luloyo, Said Baraka na Shafii Amri.
Wengine ni mjumbe wa zamani Musa Katabalo, Salim Seif, Silvester Haule, Benjamin Jackson na Hamad Islam.
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika January 13 mwaka huu baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitaka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi ikiwemo ya Manji aliyeandika barua ya kujiuzulu Mei 2017 na sasa zimeibuka tetesi kwamba anataka kurudi kwenye nafasi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles