24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Hoseah ataka mahakama ya makosa ya rushwa pekee

hoseNa Pendo Fundisha, Mbeya

 

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, amesema kitendo cha mwajiri kupewa nguvu ya kushughulikia makosa ya jinai kwa watumishi wa umma, kimekuwa kikidhoofisha mapambano dhidi ya rushwa.

Akizungumza na MTANZANIA hivi karibuni mjini hapa, Dk. Hoseah, alisema uamuzi huo umekuwa ukidhalilisha dhana nzima ya uadilifu na uwajibikaji.

Alisema yeye binafsi hakubaliani na suala hilo, na kwamba ili kuondokana nalo, ni wakati mwafaka wa Serikali kuwa na mahakama itakayoshughulikia makosa ya rushwa pekee.

“Mwajiri kapewa uamuzi mkubwa wa kushughulikia mambo ya jinai, si sahihi, uhusiano wa mwajiri na mwajiriwa ni mambo ya sheria za kazi, lazima tuwe na utaratibu mzuri hapa,” alisema.

Dk. Hoseah alisema hali hiyo, imesababisha mtumishi anapokutwa na jinai na kushtakiwa mahakamani, bado anakuwa na fursa ya kuendelea na kazi, wakati kimaadili si sahihi hata kidogo.

Alisema kutokana na changamoto hiyo, tayari ameiandikia barua Idara ya Utumishi wa Umma inayowataka viongozi kuliangalia upya suala hilo.

“Hili likiendelea kuachwa hivi, watumishi watajenga kiburi na kufanya mambo wanavyotaka, wanaamini hata kama watakutwa na makosa ya ubadhilifu wa mali ya umma, wataendelea kuwa kazini,” alisema.

Alisema, hatua ya mtumishi kutuhumiwa tu na kufikishwa mahakamani, anatakiwa  asirudi tena ofisini na kulipwa nusu mshahara hadi kesi itakapomalizika.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles