28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Array

DK. Bashiru: Ni uzembe chama tawala kutotumia dola kubaki madarakani

Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amesema endapo chama kilichopo madarakani kitashindwa kutumia dola kubaki madarakani, itakuwa ni uzembe wake wenyewe.

Dk. Bashiru alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika mahojiano na waandishi wa habari wa Kampuni ya IPP wakati alipotembelea ofisi za kampuni hiyo jana.

Alisema vyama tawala kama Kanu cha Kenya na UNIP cha Zambia vilishindwa kutumia dola na ndio maana viliondolewa madarakani.

“Unashika dola halafu unatumia dola kubaki kwenye dola, halafu akitokea mtu ambaye ana busara zaidi kukwambia usitumie dola kubaki kwenye dola ukamsikiliza na siku ukishatoka hurudi tena. Hata kwenye kazi inatafuta kazi.

“Hata Chadema au ACT-Wazalendo au CUF wakiingia madarakani watatumia dola vizuri ili wasitoke na hiyo ndio kazi yangu kama katibu mkuu wa chama tawala kazi yangu ni kuhakikisha tunaitumia dola vizuri kuhakikisha hatutoki madarakani.

Katika hilo alisema kinachotakiwa kwa chama kilichopo madarakani ni kutotumia vibaya kunyanyasa washindani wake.

“Lakini kama unataka kutumia dola kuwavuta watoke waliko waje kwako si ni sawa na kwenye vita, unateka vifaru na bunduki halafu unatumia vifaru hivyo hivyo unakwenda kushambulia. Kwa hiyo wanaosubiri sisi tulegelege katika kutumia dola, watasubiri sana huo ndio ukweli hata Trump (Rais wa Marekani, Donald Trump) leo kumwondoa ni ngumu,”alisema katibu mkuu huyo.

Dk. Bashiru alisema kuna nafuu kubwa kwa chama kilichopo madarakani kutumia nguvu za dola kufanya mambo ya kujenga imani kwa wapigakura ili kibaki madarakani, kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akitumbua watumishi wa umma na kusimamia matumizi ya fedha, kukusanya kodi na kuhakikisha chama chake kinabaki madarakani.

Kuhusu vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano ya kisiasa huku CCM ikiendelea kufanya mikutano hiyo, alisema CCM ndicho chama kilichopo madakarani hivyo lazima kitumie nafasi kutoa huduma kwa wananchi.

“Vyama vinavyoshindana kutuondoa madarakani vijue kwamba hata vyenyewe vikiingia madarakani vinahitaji nafasi ya kutoa huduma kwa umma mfano lile daraja lililoachia ya Dodoma na Morogoro leo hii zingepita siku saba bila kutengenezwa gharama ya siasa tungelipa sisi CCM,”alisema Dk. Bashiru.

Alipoulizwa kuhusu Rais John Magufuli kukutana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani Ikulu lakini wengine hawakuonekana, alisema: “Mimi sio msaidizi wa Rais, lakini ana utaratibu wake wa kukutana na makundi mbalimbali juzi wameonekana viongozi wa siasa sasa sijui wanaofuata lakini ni mwendelezo wa kukutana na makundi mbalimbali,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles