24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bashiru arusha kombora kwa Mbatia, Mbowe

Safina Sarwatt-KILIMANJARO

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na mwenzake wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), wamekuwa wakifanyakazi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.

Mbali na Mbatia, pia aliwataja wabunge Zitto Kabwe wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) na Mchungaji Peter Msigwa  wa Iringa Mjini (Chadema).

Hayo aliliyasema jana mjini Moshi, alipokuwa akizungumza na mabalozi wa mashina ambapo alisema  wabunge hao wamekuwa wakifanyakazi ya chama tawala CCM kwa sababu hawana serikali wala Ikulu  na kwa sasa wanafanyakazi kwa maelekezo ya CCM.

Pamoja na hali hiyo, alitoa onyo kwa Zitto  ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na kusema si wa viwango vyake huku akimtaka kumtomzoea.

“Mbatia ni mtu mwelewa sana sisi kama chama tutakaa nae tumpe malekezo na kwamba hatuna wasiwasi nae kabisa. Msingwa pia na Zitto hawana shida wale ni watu wetu wanaisaidia CCM kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama .

“Mbowe  tutampa malekezo,tunajua na jana nilikuwa jimboni kwake Hai , nilipokelewa vizuri na watu wake wameniahidi wako tayari,” alisema Dk. Bashiru

Aliwataka wananchi waendelee kuchapa kazi ili kujenga uchumi wa nchi na katu waepuke kuishi maisha ya anasa.

Alisema  majimbo saba ya Mkoa wa Kilimanjaro  yote yamekuwa ya CCM, hata wapinzani wanalitambua hilo.

Alisema  majimbo ya  Moshi Mjini ,Vunjo, Moshi Vijijini, Same Mashariki na Rombo hayo ni majimbo yaongozwa na upinzani, yatarudi CCM kwa sababu wakuu wa wilaya ni wa  chama hicho na Serikali.

Alisema chama hicho hakijaahidi  kuwagawia wananchi fedha zaidi ya maendeleo kwa wananchi.

 Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya alisema  uchaguzi ujao, chama hicho kitashinda majimbo yote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles