27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

DJOKOVIC AJITOA KUSHIRIKI TENISI 2017

BELGRADE, SERBIA


BINGWA namba nne kwa ubora wa mchezo wa tenisi duniani, Novak Djokovic, ametangaza kujitoa kwenye michuano mbalimbali msimu huu kutokana na kusumbuliwa na kiwiko cha mkono.

Bingwa huyo raia wa nchini Serbia, amekuwa kwenye kipindi kigumu msimu huu kwa miezi minne iliyopita, kutokana na kusumbuliwa na maumivu makali kwenye mkono wake wa kulia, hivyo ameweka wazi ni bora apumzike ili kupata matibabu.

Hata hivyo, kujitoa kwake kwenye michuano msimu huu itamfanya ashuke kwenye viwango vya ubora na kuna uwezekano mkubwa akawa nje ya nafasi 10 bora hadi pale atakaporudi kwenye mchezo mwakani.

“Madaktari wangu wote wamekuwa wakinishauri nipumzike msimu huu wote kutokana na hali yangu ya kifundo cha mkono, nimekubaliano nao kwa kuwa wao ni wataalamu.

“Najua mapumziko yangu yatanifanya nikose baadhi ya michuano msimu huu, lakini sina jinsi, inabidi iwe hivyo, kutokana na hali yenyewe, lakini ninaamini nitarudi kwenye ubora ule ule kwa kuwa nitaendelea na mazoezi ya kujiweka vizuri.

“Japokuwa nipo kwenye kiwango cha hali hii, lakini kuna baadhi ya mambo nilikuwa sijayafanyia kazi, hivyo katika kipindi hiki cha mapumziko nitahakikisha ninavifanyia kazi.

“Kukaa miezi mitano kuanzia sasa ni safari ndefu, lakini inabidi iwe hivyo, ili nizidi kuwa bora nikirudi msimu ujao, hata hivyo, kipindi hiki cha mapumziko nitakuwa na furaha kubwa kwa kuwa ninatarajia kupata mtoto kwa mara ya pili.

“Mimi na mke wangu, Jelena tunatarajia kuongeza familia hivi karibuni, hivyo siwezi kujutia nafasi hii ya mapumziko, nitakuwa tayari kwa jambo lolote,” alisema Djokovic.

Baadhi ya michuano mikubwa ambayo ataikosa mchezaji huyo katika kipindi hiki cha mapumziko yake ni pamoja na US Open, itakayofanyika Agosti 28 hadi Septemba 10, Davis Cup, Septemba 15 hadi 17, Serbia dhidi ya France, ATP Tour Asian swing, Septemba 25 hadi Oktoba 15, BNP Paribas Paris Masters kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 6, ATP Tour Finals kuanzia Novemba 13 hadi 19, huku Novemba 24 hadi 26 michuano ya Davis Cup kwa makundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles