24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DIWANI MUNISI AONYA WANANCHI WANAOTOA TAARIFA ZA UCHOCHEZI

Mwandishi Wetu, Moshi

Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Martini Munisi amewaonya baadhi  ya wananchi katika kata hiyo wanaotoa taarifa za uchochezi na kupotosha kwani zinachafua sifa ya kijiji chao.

Munisi ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wake na wananchi wa Kitongoji cha Maanga, kutokana na malalamiko ya wananchi hao kutokuwa na uhusiano mzuri kati yao na askari wa Kinappa katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Kutokana na hali hiyo, amesema yeye kama kiongozi wa kata hiyo hatalifumbia macho suala la wananchi kuharibu hifadhi hiyo.

“Lakini pia siko tayari tayari kuona wananchi wangu wananyanyaswa na askari hao wa Kinappa, lakini pia ni lazima tutambue ni jukumu kila mwananchi kutoa taarifa za kweli  kwani endapo mtaendelea kutoa taarifa hizo za uchochezi  nitachukua hatua ya kuwaita askari hao wa Kinappa ili wajibu  hayo yanayosemwa na baadhi ya wananchi hao,” amesema Munisi.

Mmoja wa wananchi wa kitongoji hicho anayejitambulisha kwa jina la Bethel Sawe amesema kwa zaidi ya miaka 10 hakuna mwananchi yeyote ambaye amejihusisha na upasuaji wa mbao za kemfa na mpodo ndani ya hifadhi hiyo.

“Kinappa wameweka watu wasio waaminifu kwani wamekuwa  wakitoa taarifa ambazo hazina ukweli jambo linalosababisha matatizo kwa baadhi yetu kukamatwa bila kosa,” amesema.

Naye mkazi mwingine, Ndata Mushi amesema watu wanakamatwa nje ya hifadhi na kukamatishwa magogo ya miti kwa lazima jambo ambalo si haki kwao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles