24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DIWANI CHADEMA AWAANGUKIA WADAU

NA GUSTAPHU HAULE, PWANI

DIWANI wa Kata ya Mailimoja katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Ramadhani Lutambi (Chadema), amewaangukia wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kuwaomba wajitokeze kuchangia ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Muheza.

Lutambi alitoa ombi hilo juzi alipokuwa akizungumza na MTANZANIA jana wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa shule hiyo unaoendelea kufanyika katika Mtaa wa Muheza chini ya nguvu za wananchi.

Alisema kwa muda mrefu Mtaa wa Muheza haukuwa na shule ya msingi, jambo ambalo ni kero kwa wanafunzi wa eneo hilo kwa kuwa wanalazimika kutembea umbali wa kilomita tano mpaka kufika Shule ya Msingi Mailimoja.

Alisema kutokana na adha hiyo, wananchi wa mtaa huo kwa pamoja walikubaliana kuanza kujenga shule hiyo ambapo kwa hatua ya awali, wameanza na madarasa matatu ili kuwaokoa watoto wadogo ambao wamekuwa wakiteseka kutembea.

“Shule hii inajengwa na nguvu za wananchi wenyewe kwa makubaliano yao, wameanza na madarasa haya matatu, ni vyema Serikali na wadau wengine tukashirikiana na wananchi hawa katika kukamilisha jambo hili ambalo ni faida kwa jamii ,” alisema Lutambi.

Alisema  lengo ni kuhakikisha mpaka ifikapo Desemba mwaka huu, shule hiyo iwe imekamilika, lakini kutokana na changamoto zilizopo ni vyema wadau wakajitokeza kuchangia.

Aliwaahidi wananchi wa Mtaa wa Muheza kuwa yupo tayari kuchangia ujenzi wa shule hiyo kwa faida na maendeleo ya wananchi wake na kwamba atashiriki katika hatua zote ili kuhakikisha Shule hiyo inakamilika kwa wakati.

Katibu wa Tawi la Muheza kupitia Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Getrude Kapinga, alisema wameweka kando itikadi zao na kushirikiana katika ujuenzi wa shule hiyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles