DIMPOZ KUDONDOSHA CHECHE MWANZA

0
3

Na CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya mashabiki wa muziki nchini kuisubiri kwa hamu video ya wimbo mpya wa Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ unaoitwa Cheche, msanii huyo chini ya uongozi wa Lebo ya Rock Star 4000 inayoongozwa na Ali Kiba leo anatarajia kuiachia katika Tamasha la Fiesta kwenye Viwanja vya CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Dimpoz ameiambia ShowBiz kuwa ni muda mrefu umepita hajatumbuiza kwenye jukwaa lolote hapa Bongo hivyo ameamua kufanya onyesho hilo na kuzindua video ya Cheche ili kukata kiu ya mashabiki.

“Video ilikuwepo muda mrefu sema nilikuwa natafuta muda mzuri wa kuitoa, naitoa Jumamosi (leo) pale CCM Kirumba na hii ndiyo kazi yangu ya kwanza nikiwa chini ya uongozi wangu wa RockStar 4000,” alisema Dimpoz.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here