DIEGO MARADONA APATA TIMU MEXICO

0
510


CULIACAN, MEXICO

Bingwa wa soka kutoka Argentina, Diego Maradona, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Dorados de Sinaloa ambayo inashiriki Ligi Daraja la Pili nchini Mexico.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 1986 akiwa na Argentina, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 57, aliwahi kupewa nafasi ya kuifundisha timu hiyo ya taifa lake tangu mwaka 2008 hadi 2010, lakini hakulipa mafanikio makubwa.

Hata hivyo, mara ya mwisho kufundisha soka ilikuwa klabu ya Al-Fujairah, iliyopo katika Umoja wa Falme za Kiarabu na mkataba wake ulimalizika Aprili mwaka huu.

Vyombo vya habari nchini Mexico vinadai kuwa, Maradona ameajiriwa na klabu hiyo mpya kwa ajili ya kuchukuwa nafasi ya Francisco Gamez, aliyefutwa kazi Alhamisi.

Klabu hiyo imesambaza video fupi inayoonesha kumkaribisha kocha huyo mpya huku wakisema ‘Karibu Diego Timiza 10’ hiyo ni namba ambayo iliyokuwa kwenye jezi ya Maradona alipokuwa mchezaji.

Klabu ya Dorados ilianzishwa mwaka 2003 na kocha wa sasa wa Manchester City, Pep Guardiola, aliwahi kuichezea kwa miezi 6 mnamo mwaka 2005.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here