Imechapishwa: Wed, Feb 7th, 2018

DIAMOND: SIONI SABABU YA KUCHUKIANA

NA BRIGHITER MASAKI


MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amefunguka na kusema huu si muda wa kuwa na chuki na wasanii wenzake, ila ni muda wa kushirikiana.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache baada ya kuonekana akimkaribisha mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu, katika utambulisho wa msanii mpya wa WCB, Malomboso.

Diamond alisema, wapo watu ambao wanapenda kuwaona baadhi ya wasanii wakiwa kwenye vita ambayo haina sababu za msingi.

“Wengi wanapenda kuona watu wakiwa kwenye mgogoro, kuna mtu aliniambia kwamba ‘dogo mimi shabiki yako mkubwa na nakukubali sana, ila kitendo cha kumwalika Wema umenichukiza.

“Naweza kusema wapo ambao wanapenda kutuona tukiendelea kuwa kwenye mgogoro, maisha hayapo hivyo, kila kitu kina mwanzo na mwisho,” alisema Diamond.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

DIAMOND: SIONI SABABU YA KUCHUKIANA