27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond ahamasisha wanafunzi kujikinga na ukimwi

Anna Potinus

Kuelekea tamasha la Wasafi (Wasafi festival), msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametembelea Shule ya Msingi Mwongozo kwaajili ya kutoa msaada na elimu ya virusi vya ukimwi ambapo aliambatana na wasanii watakaotumbuiza katika taamasha hilo.

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi Novemba 7, mbapo baadhi ya shule za sekondari za jirani zimehudhuria ambazo Shule ya Sekondari ya Kambangwa Shule ya Sekondar Hananasifu, Shule ya Sekondari Turiani, Shule ya Sekondari Mzimuni na Shule ya Sekondari Makumbusho.

Aidha Diamond ameambatana na wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Jumamosi Novemba 9ambapo kati yao ni Khadija Kopa, Nyoshi El Sadat, Mboso, Queen Darleen, Rayvanny, Amber Lulu.

Akizungumza na wanafunzi hao Diamond amewataka kuongeza juhudi katika masomo yao na kujiepusha na mambo mabaya ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Wasanii wengi wanatokea katika Wilaya ya Kinondoni hivyo jitahidini muyashikilie mazuri kuliko mabaya, mkitaka kufaniikiwa zingatia katile unachokifanya, hapa kuna historia ya mambo ya mihadarati nisingependa kuwaona na nyie mkiingia huko,” amesema Diamond.

Kwa upande wake Mratibu wa Shughuli za kudhibiti ukimwi Halmashauri ya Kinondoni, Roby Gweso amewataka wanafunzi kuachana na tabia ya kutumia madawa ya kulevya na kuepuka vishawishi ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles