28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Deni lilikwamisha video ya Timbulo

GLORY MLAY

MSANII wa Bongo Fleva, Ally Timbulo, amesema alipoteza moja ya video yake kutokana na kushindwa kulipa deni la sh.15, 000.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Timbulo alisema ilikuwa ndio video yake ya kwanza kwenye muziki wa bongo fleva, lakini kiasi hicho cha fedha kilimkwamisha kuipata video hiyo.

“Kwanza nilipata changamoto ya kupata fedha ya kutengeneza video hiyo ambayo nilikuwa sijaipa hata jina, nikamuomba mwaandaaji anipe ili baada ya kuingia sokoni niweze kumlipa kwa kuwa ningeweza kupata fedha, lakini alikataa kabisa.

“Nilijua ananitania lakini siku zinalivyozidi kwenda nikawa namtafuta simpati na nikienda studio kwake simkuti hivyo video hiyo ikapotea kwa sababu ya sh.15, 000 tu,” alisema msanii huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles