27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Deni la wakulima wa pamba Simiyu sasa labaki bil/- 1

Derick Milton, Simiyu

Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Simiyu imesema kuwa wakulima wa pamba katika mkoa huo bado wanadai kiasi cha Sh bilioni 1.1 kutoka kwa makapuni sita kati ya 19 ambayo yalinunua zao hilo msimu wa mwaka 2019/20.

Akitoa taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka 2020 ya utendaji kazi wake kwa waandishi wa habari Mkuu wa taasisi hiyo, Joshua Msuya amesema kuwa kampuni yenye deni kubwa ni NGS ambayo inadaiwa Sh milioni 810.

Amezitaja kampuni nyingine kuwa ni Matongo inayodaiwa Sh milioni 217 pamoja na Nsagali Ivestement Sh milioni 20.8, huku makapuni mengine matatu yakidaiwa kiasi kidogo cha pesa ambacho hakukitaja.

Amesema kuwa awali deni la wakulima lilikuwa bilioni 4.5 na baada ya taasisi hiyo kuingilia kati kiasi cha Sh bilioni 3.4 kimelipwa kwa wakulima ndani ya muda huo wa miezi mitatu.

“Bado makampuni hayo na mengine ambayo yamemaliza madeni ya wakulima wanadaiwa ushuru wa vyama vya msingi vya ushirika kiasi cha sh. bilioni 4.3 lakini pia hata halmashuari bado nazo zinadai ushuru wake,” amesema Msuya.

Aidha ameyataka makampuni hayo kuhakikisha yanalipa madeni hayo ya wakulima kama maagizo ya serikali yalivyo, huku akihaidi kuwa taasisi hiyo itahakikisha kila mkulima analipwa fedha zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles