27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

De Bruyne ahofia familia yake kupata corona

MANCHESTER, ENGLAND 

KIUNGO wa timu ya Manchester City, Kevin De Bruyne, amedai alikuwa na wasiwasi familia yake kupata maambukizi ya virusi vya corona baada ya watoto na mke wake kuugua kwa siku zinazofuatana.

Hali hiyo ilitokea mara baada ya nchini Uingereza kutangaza watu kukaa ndani kutokana na virusi hivyo kuenea kwa kasi, lakini kwa sasa wote wapo sawa.

Mchezaji huyo raia wa nchini Ubelgiji amedai baada ya kuona hali hiyo aliamua kujitenga na familia yake kwa kuhofia kupata maambukizi.

“Mwanzoni mwa watu kuambiwa wasitoke nje familia yangu walikuwa wagonjwa kwa siku nane au tisha, alianza kuugua mtoto wangu mdogo, akafuata mwingine baada ya hapo akaja mke wangu, lakini sikuwa najua kama ni virusi vya corona au ugonjwa mwingine.

“Lakini jambo jema ni kwamba wote wapo sawa kwa sasa baada ya wiki mbili au tatu, nilidhani ilikuwa corona, lakini kama ingekuwa hivyo basi hali zao zingekuwa mbaya zaidi,” alisema mchezaji huyo.

Ligi nchini humo na sehemu zingine mbalimbali zimesimama kwa kuhofia kuenea kwa virusi hivyo, lakini wachezaji wamepewa program zao za kufanya hata wakiwa nyumbani kwa ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya kuendelea na ligi mara itakapotangazwa.

De Bruyne yeye amesema tangu ligi yao isimame bado anaendelea kujifua kwa ajili ya kuipigania timu yake kwa michezo iliobaki pamoja na yeye mwenyewe kujiweka sawa.

“Wiki mbili za mwanzo bado sikuwa sawa kutokana na mwenendo wa virusi vya corona, lakini kwa sasa natumia muda mwingi kufanya mazoezi kwenye bwawa la kuogelea pamoja na kukimbia, hata hivyo mazoezi mengine mengi ninayafanya kulingana na program, kila mmoja anaamini hali itakuja kuwa sawa na mambo mengine yataendelea,” alisema mchezaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles