30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DCB yazindua akaunti ya muda maalumu

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

BENKI ya Biashara ya DCB, imezindua bidhaa maalumu kwa ajili ya wateja wa akaunti ya muda maalumu (Fixed Deposit) ijulikanayo kama ‘DCB LAMBA KWANZA’.

Bidhaa hiyo mpya itamwezesha mteja wa DCB kuwekeza hadi miaka miwili na kupata riba ya hadi asilimia 14 ya amana atakayowekeza na riba ya mwezi italipwa papo hapo pindi anapofungua akaunti. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko, alisema akaunti hiyo itamwezesha mteja kupata riba kila mwezi, hivyo kufanya wateja wa DCB kufurahia maisha kwani kila mwezi ni wa faida.

“Riba inalipwa mwanzo wa kila mwezi, malipo ya riba ni rafiki mteja anaweza kuwekeza kuanzia miezi mitatu mpaka miaka miwili. Ni matumaini yetu wateja wetu watafurahia akaunti hii kwani tumeboresha maisha na uchumi,” alisema.

Alisema lengo kubwa la kuanzishwa kwa akaunti hiyo ni kuwapa fursa wateja wa DCB kuweza kuwekeza kwa faida na manufaa. 

“Tumekuja na jina hili la ‘DCB Lamba Kwanza’ kama lilivyo neno lenyewe, mteja wetu ataweza kulamba riba ya mwezi papo hapo pindi atakapofungua akaunti,” aliongeza mkurugenzi wa biashara.

Ngaluko alisema akaunti ya DCB Lamba Kwanza haina ‘stress’ kwani itamwezesha mteja kupata kipato kikubwa kila mwezi kwa kipindi kirefu, hivyo kuitofautisha na akaunti nyingine kama hizi,” alisema.

“Mteja anaweza kufungua akaunti katika tawi lolote la DCB ama kupitia huduma za kidigitali kwa kupiga *150*85# huku mteja akihakikishiwa usalama wa fedha zake, wakati huo huo hakuna makato ya akaunti ya kila mwezi na hakuna gharama ya kufungua akaunti.

“Uboreshaji huduma na mahusiano ya wateja umekuwa ndio kigezo kikuu katika kuongeza amana nafuu na za muda mrefu hasa kutoka kwa wanahisa waanzilishi na mashirika mbalimbali yaliyoendelea kuwekeza na Benki ya DCB,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles