30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DC: Nitawasaka wanaomkashifu Rais

Richard Kasesela
Richard Kasesela

NA RAYMOND MINJA, IRINGA

MKUU wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, amesema kamati ya ulinzi na usalama haitaruhusu mikutano ya hadhara itakayoombwa na vyama vya siasa wilayani humo.

Pamoja na uamuzi huo, Kasesela amesema kamati hiyo itawasaka na kuwafikisha katika vyombo vya dola watu wanaomkashifu Rais Dk. John Magufuli na viongozi wengine wa Serikali.

“Tuendelee na majukwaa ya utendaji, mipasho ya siasa tupumzike ili tuiache Serikali ifanye kazi zake,” alisema.

Alisema uchaguzi mkuu mwaka jana umepita kwa kumpata Rais, wabunge na madiwani, hakuna sababu tena ya kuendelea na mikutano ya kisiasa kila kukicha.

“Kama tunataka mbwembwe za siasa majukwaani, tusubiri uchaguzi wa Serikali za Mitaa au uchaguzi mkuu wa 2020,” alisema.

Alisema hatakuwa na msalia mtume na mtu yeyote awe mwana Chadema au CCM, atakayethubutu kunyanyua mdomo na kumtusi kiongozi yeyote au mwanachama mwenzeke, atakula naye sahani moja ili kuheshimiana na kutii mamlaka zilizo madarakani.

Wakati huo huo, amewataka viongozi wa taasisi mbalimbali za dini ambazo hakuzitaja kumaliza migogoro yao ya uongozi inayoelekea kuhatarisha amani ya wilaya.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdala, ameahidi kuzishughulikia changamoto mbalimbali za kimaendeleo wilayani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles