31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DC Kilolo apiga marufuku wajawazito kutozwa faini

                          Raymond Minja, Iringa



Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah, amepiga marufuku wajawazito kutozwa faini pindi waendapo  kujifungua kwenye zahanati  kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sera ya afya na kumuongezea mzigo mwananchi.

Marufuku hiyo imekuja mara baada ya mmoja wa wakinamana wa Kijiji cha Wangiwete kata ya Masisiwe wilayani humo Ageria Abel kutoa kilio hicho kwa mkuu huyo wa wilaya wakati wa ziara yake ya kata kwa kata na kijiji kwa kijiji ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

“Mkuu wa wilaya tunashukuru kwa kuja umejionea mwenye miundombinu ya barabara  ilivyo mibovu sisi akina mama sio kwamba tunapenda kujifungulia nyumbani ila uchungu unakushika unaita gari mpaka ifike  tayari mama ashajifungua na ukimpeleka kituoni baadae  analipishwa faini tunakuomba utusaidie, “amesema Abel.

Abdallah amesema faini hiyo ambayo wamekuwa wakilipishwa wakinamama hao pindi  wanapochelewa kufika kituo cha afya kwa ajili ya kujifungua haiko kisheria hivyo inapaswa kuachwa.

“Mtendaji nakuagiza kuanzia leo ni marufuku kuwatoza wajawazito hiyo siyo sera ya afya,  mazingira sio rafiki ile zahanati yetu pale ambayo wanapata huduma akinamama hawa  naamini mambo haya yatakwisha na huduma ya kujifungua,matibabu kwa wazee kuanzia miaka 60 na watoto chini ya miaka mitano ni bure,”amesema.

Hata hivyo Abdallah amewataka wananchi hao kuendelea kujenga majengo ya zahanati na shule ili serikali iweze kumalizia na kuleta watumishi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadae na hospitali ya wilaya ya Kilolo itakapokamilika changamoto ya afya na vifo vya  wajawazito na watoto itakwisha kwani watapata huduma karibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles