24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DC apongeza usimamizi wa elimu Kinondoni

Brighiter Masaki, Dar Es Salaam

Mkuu Wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amewaagiza wakuu wa shule zote za Sekondari katika Halmashauri hiyo kuacha mara moja tabia ya kuwazuia wanafunzi wanaojiunga na kidato cha chanza kuanza masomo kutokana na kutokamilisha mahitaji yao ya shule.

Chongolo ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu kwa ufaulu mzuri wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 iliyofanyika katika viwanja vya Polisi Officers Mess Masaki.

“Zipo baadhi ya shule ambazo zinawazuia wanafunzi kujiunga na masomo kutokana na kutokamilisha mahitaji ya shule na kusema kuwa bado hajasikia jambo hilo likifanyika katika Halmashauri ya Kinondoni na hivyo kutumia nafasi hiyo kuwaonya wasithubutu kufanya hivyo” alisema Chongolo.

Aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano inatoa elimu bila malipo na kwamba suala la kuchelewa kukamilisha mahitaji hayo isiwe sababu ya kuwazuia watoto hao wa wanyonge kushindwa kuanza masomo yao.

“Kuna baadhi ya maeneo nimesikia kuna wakuu wa shule wanawarudisha nyumbani watoto kwa sababu hawajakamilisha mahitaji yao, kama mtoto hana viatu, sijui nini waache wasome wakati wazazi wao wanawatafutia mahitaji hayo, naomba nisikie mwanafunzi amerudishwa nyumbani kwenye wilaya yangu” amesisitiza Chongolo.

Aliongeza kuwa Halmashauri hiyo imefanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 kwa kuwapa ufaulu wa asilimia 97.17 ambapo imekuwa ya tatu kati ya Halmashauri 186 kitaifa kwa jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 12,619, wavulana 6,115 na wasichana 6,450, huku waliofanya wakiwa 12,523 ,wavulana 6,058 na wasichana 6,465.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles