DC apinga dawa za pamba kutolewa bure kwa wakulima

0
524

Derick Milton, Bariadi

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga ameungana na wakulima wa zao la pamba wilayani humo kutaka kubadilishwa kwa utaratibu wa dawa za kuua wadudu kutolewa bure na badala yake ziuzwe.

Ametoa kauli hiyo Leo Jumatatu Machi 25, wakati akiongea na wakulima wa pamba, viongozi vyama vya ushirika, watendaji wa vijiji na mtaa pamoja na maafisa kilimo katika kikao kazi kilichofanyikia mjini Bariadi ambapo amesema kuwa bodi ya pamba imeshindwa kuweka vizuri utaratibu huo, ambapo wakulima wamekuwa wakiangaika kupata dawa huku pamba yao ikiendelea kushambuliwa na wadudu.

“Huu utaratibu wa dawa kutolewa bure umeleta shida nyingi, wagawaji wamekuwa wakitukanwa na wakulima kwa kuwapatia dawa chache, ni vyema dawa zikauzwa kama ilivyokuwa zamani, lakini utaratibu huu bodi wameshindwa,” amesema

Katika kikao hicho baadhi ya wakulima waliitaka serikali katika msimu ujao wa pamba, mbegu pamoja na dawa wauziwe kama ilivyokuwa zamani kuliko kupewa bure.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here