23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DC akemea wanafunzi wa kike kutongoza wavulana

SAM  BAHARI – SHINYANGA.

WADAU wa elimu Mkoa wa Shinyanga wamekemea  tabia ya wanafunzi wa kike wanaosoma shule za msingi na sekondari  kuwatongoza wavulana kwa lugha ya kuvutia na  yenye  kushawishi  kushiriki vitendo vya mapenzi.

Licha ya kuibuka tabia hiyo, wadau wameiomba Serikali kupitia upya sheria inayosimamia  wanafunzi  wa kike wanaopewa mimba na kukatisha masomo yao.

Akizungumza wakati wa kikao cha kutangaza matokeo ya darasa la saba juzi,  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba alisema imebainika wanafunzi wa kike kipindi hiki wameanza  kuwatongoza  wavulana na kufanya ngono  isiyo salama na mwisho wa siku hupata ujauzito.

Alisema wasichana  kuamua kubadilika tabia na kuanza kuwatongoza  wavulani, ni kutokana na ulegevu wa sheria inayotumika kwa watu wanaowapa mimba hukamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani tofauti na mtoto wa kike ambaye hubaki huru.

“Sheria hii inayohusu wanafunzi wetu wa kike kupewa mimba, inatafasiri   mwanaume aliyempa mimba mwanafunzi akamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili,  lakini mtoto wa kike anayetiwa mimba hubaki huru,”  alisema.

Akitangaza  ufaulu wa matokeo ya mitihani wa darasa la saba, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albart  Msovela alisema kwa mara ya kwanza mkoa huo umeshika nafasi ya 17 kitaifa.

Alisema mkoa uliandikisha watoto 40,292 kuanza darasa la kwanza mwaka 2013 na waliosajiliwa kufanya mtihani wa mwisho kuingia kidato cha kwanza mwaka 2020, ni 30,393 na waliofaulu ni 23,634 sawa na asilimia 77. 76.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles