24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DAWA ZA ASILI KUMI ZINAZOTIBU KIKOHOZI

KIKOHOZI ni ugonjwa unaowapata watu karibu wote, hali ya muwasho kooni pamoja na kuziba kwa baadhi ya sehemu za kupumulia puani, ubongo hutambua kuwa kuna hitilafu katika mwili.

Kukohoa pia kunaweza kuwa ni matokeo ya maambukizi ya virusi, homa, kuvuta sigara au matatizo ya kiafya kama pumu, kifua kikuu na kansa ya mapafu.

Baadhi ya dalili za kikohozi ni muwasho kooni, maumivu ya kifua na msongamano mapafuni.

Badala ya kutumia dawa za viwandani kutibu kikohozi, unaweza kujaribu mojawapo ya hizi dawa za asili za kikohozi ambazo zinapatikana kirahisi jikoni kwako.

  1. Binzari (Turmeric)

Dawa hii ya asili inao uwezo wa kutibu kikohozi, hasa kikohozi kikavu.

Weka kijiko kidogo kimoja cha unga wa binzari ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha maji ya moto, ongeza ndani kijiko kidogo cha pilipili manga ya unga.

Nusu kijiko cha chai cha unga wa mdalasini na kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi, koroga vizuri na unywe mchanganyiko huu wote kutwa mara moja kila siku mpaka umepona.

2. Tangawizi

Tangawizi ni moja ya dawa maarufu kwa kutibu kikohozi.

Tengeneza chai ukitumia tangawizi mbichi na ndani yake utumie asali na siyo sukari kwenye hii chai yako.

Kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 kila siku mpaka utakapopona.

Angalizo, usitumie dawa hii kama una ujauzito mchanga chini ya miezi minne na hata ukiwa na ujauzito zaidi ya miezi minne basi tumia kikombe kimoja tu kwa siku.

Unaweza pia kutengeneza juisi ya tangawizi freshi ukiongeza parachichi ndani yake na unywe kwa mtindo huo huo wa chai hapo juu.

  1. Limau

Limau linaweza kutumika kwa namna nyingi katika kutibu kikohozi.

Limau zina sifa za kuondoa maambukizi, pia lina vitamini muhimu ambayo hupigana na maambukizi na kukuongezea kinga ya mwili, vitamini mhimu sana, vitamini C.

Changanya vijiko vikubwa viwili vya maji ya limau na kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi na unywe mchanganyiko huo mara mbili kwa siku ndani ya siku kadhaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles