DAVIDO JUKWAA MOJA NA J. COLE, NELLY

0
472NORTH CAROLINA, MAREKANI

STAA wa muziki Afrika, David Adeleke maarufu kutoka nchini Nigeria, Davido, ametangaza kuwa, anatarajia kupanda jukwaa moja na mastaa wa muziki nchini Marekani, J. Cole, Nelly Young Thug pamoja na Big Sean.

Wasanii hao watakutana kwenye tamasha la Dreamville Festival, ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 15, huko North Carolina nchini Marekani.

Msanii huyo raia wa nchini Nigeria, ametumia ukurasa wake wa Twitter na kudai kuwa, ndoto zake zinatimia kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani.

Wasanii hao ambao watapamba tamasha hilo ni pamoja na J Cole, Big Sean, Bas, Nelly, Young Thug, Teyana Taylor na wengine wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here