26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

DARTS CHALENJI KUANZA DESEMBA MOSI

NA GLORY MLAY-DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Chama cha Darts cha Tanzania (Tada), Subira Waziri, amesema mashindano ya Darts ya Chalenji Afrika Mashariki (EADF), yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba mosi hadi 3 mwaka huu mkoani Arusha.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Subira alisema, maandalizi ya mashindano hayo ambayo yameandaliwa na chama hicho yanaendelea, huku yakitarajiwa kuhusisha mchezaji mmoja mmoja na wachezaji wawili wawili.

Amesema kuwa michuano hiyo mikubwa itashirikisha nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo wenyeji ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Alisema yatashirikisha timu za taifa na klabu za nchi za Afrika Mashariki.

Amesema mashindano hayo hufanyika kila mwaka, ambapo bingwa mtetezi ni timu ya Kenya iliyoibuka mshindi mwaka jana.

Alisema kiingilio cha mashindano  kitakuwa ni shilingi 10,000 kwa mchezaji mmoja, huku wachezaji wawili wakilipa 20,000, timu za wanaume zitalipa 50,000, wanawake 30,000 na wageni wa nchi za nje watatakiwa kulipa 200,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles