30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

…DARASSA NI MFANO, WAPO WENGI KWENYE GEMU!

Na RAMADHANI MASENGA

MUZIKI unahitaji utulivu, umakini na taimingi. Msanii ili atoe nyimbo nzuri hapaswi kuwa na pupa wala kuendekeza presha ya mashabiki. Akishindwa kufanya hivyo, lazima ataanguka.

Usidhani Mb Dog kaishiwa. Bado Mb Dog ni yuleyule. Msanii mkali mwenye sauti tamu na mashairi adimu. Ila Mb Dog sasa hatambi kwa sababu wakati akiandika, anafikiria nyimbo kama Latifa, Inamaana na Si Ulinambia.

Akiwa na fikra hizi anajikuta anaweweseka na kutoa nyimbo ya hovyo. Msanii ili atoe nyimbo nzuri anatakiwa kuwa na mawazo halisi yatakayowasilisha hisia zake vizuri.

Katika hili wasanii wengi wamefeli. Juma Nature kaanguka, Inspekta Haroun hajiwezi na Afande Sele hajui afanye nini. Msanii aliyeweza kukaa kimya na kutoa nyimbo inayoendana na wakati huu ni Jay Moe. Unajua kwanini?

Jay Moe hakuwa na presha. Alikaa, akafikiri akawasilisha hisia zake bila tabu. Matokeo yake watu wanashangaa ni kwanini bado ni lulu japo ni miaka mingi imepita toka awe katika game.

Namuona Darassa akipata tabu kurudi katika ukali wake. Kabla ya nyimbo ya muziki, Darassa alitoa nyimbo kadhaa nyuma na zikafanya vizuri.

Nyimbo kama Too Much, Heyaheya na Sikati Tamaa zinatosha kuonesha uhalisia. Sasa baada ya nyimbo hizo na muziki kufunika rekodi za muziki wa Hip Hop kwa miaka ya karibuni, Darassa anagwayagwaya kurudi katika chati za muziki.

Katoa nyimbo ila ni kawaida sana. Kajaribu kupita mlemle alipopita katika nyimbo ya muziki. Hesabu hii ilikuwa mbaya mno.

Watu hawakupenda nyimbo ya muziki kwa sababu tu ya biti na melodi. Nyimbo ya muziki ilipendwa kwa sababu ya mashairi, biti, melodi na wakati.

Hapa ndipo alipochemka Darassa. Ila huwezi kumlaumu sana. Sio yeye tu aliyeingia katika mtego huu baada ya nyimbo ya awali kutamba sana. Wapo wengi. Nuruwell anatosha kuwa mfano.

Baada ya nyimbo ya muziki kutamba Darassa aliingia katika dunia ya wasiwasi. Dunia ya kutaka kutoa nyimbo kali kuzidi Muziki. Mwanamuziki akiwa katika hali hii hawezi kufanya vizuri.

Muziki ni tofauti na kazi nyingine. Ili mwanamuziki atoe nyimbo kali inabidi asikilize hisia zake. Badala ya kufanya hivi, Darassa alikuwa akisikilizia mashabiki wanataka nini. Matokeo yake katuchekesha kwa nyimbo badala ya kutuburudisha.

Kwanza ajiulize, wakati akitoa Muziki alitegenea itakuwa kubwa namna ilivyokuwa? Anajua ni kwanini? Yes, ni kwa sababu wimbo mzuri. Nini kilimsukuma kutunga nyimbo ya namna ile?

Hisia na fikra zilizomtuma kuandika nyimbo ile ndizo zinatakiwa kumtuma kutoa nyimbo nyingine. Aache kujidanganya kwamba kupita alipopita katika muziki nyimbo itakuwa kali. Yeye ni mwanamuziki mzuri.

Hatakiwi kuishi kwa kukariri. Afanye kama ambavyo amekuwa akifanya. Afanye bila kufikiria nyimbo alizotoa. Asikilize hisia zake na ajue nyimbo anayotakiwa kutoa inabidi aanze kuipenda yeye mwenyewe kwanza.

Yeye ni miongoni mwa watu watakaosikiliza wimbo atakaotoa. Hivyo ianze kumburudisha yeye. Naamini huu wimbo mpya alioutoa hata yeye mwenyewe hauelewi.

Naamini aliitoa kwa ajili ya mashabiki kupenda. Mashabiki ambao hakuwafikiria wakati anatoa wimbo wa awali. Ajitafakari.

Bob Marley aliwahi kusema ili wimbo utambe inatakiwa itambe kwanza chumbani mwako. Alimaanisha kuwa kabla hata ya kwenda studio kurekodi, inabidi kwanza umburudishe msanii husika.

Wasanii wengi hili hawana. Wengi wanaandika wakiwaza nyimbo zao za awali ama mamilioni wanayoingiza makundi makubwa nchini kwenye muziki.

Kwa fikra hizi, hisia za msanii haziwezi kuleta kitu mwafaka. Ili Darassa aweze kurudi katika chati hatakiwi kutoa nyimbo kwa shinikizo. Atulie, ajipange kisha asikilize hisia zake ambazo zimekuwa zikimtuma kuandika mashairi.

Bila kufanya hivyo atapotea kama walivyopotea kina K Sal na Makamua. Muziki ni kazi na burudani. Msanii akifanya muziki kama kazi zaidi na kusahau kuwa ni burudani ambayo inapaswa ianze kumburudisha mwenyewe, lazima achemke!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles