27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DAMU YADAIWA KUUZWA HOSPITALI YA HAYDOM


Na MWANDISHI WETU- MANYARA   |

BAADHI ya wafanyakazi wa Hopitali ya Haydom mkoani Manyara, wamelalamikiwa kwa kuwauzia damu wagonjwa wanaokwenda kwa ajili ya matibabu.

Hospitali ya Haydom inamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mbulu na ilianzishwa mwaka 1955 na wamisionari kutoka Norway.

Mbali ya biashara ya damu kufanyika hospitalini hapo na uongozi wa taasisi hiyo kukiri, pia inakabiliwa na matatizo kadha wa kadha ya uongozi ikiwamo mawasiliano duni ya utendaji kati ya menejimenti na Bodi ya Wadhamini.

Kutokana na matatizo ya uongozi (kama itakavyobainishwa kwenye ripoti kamili), imethibitika malalamiko mengi ya wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hiyo kubwa kaskazini mwa Tanzania, huwa yanaishia kwenye menejimenti ya hospitali pekee.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Haydom, Dk. Emanuel Nuwass, alikiri tatizo la kuuzwa damu hospitalini hapo, na kusema ‘biashara’ hiyo inafanywa na watumishi wachache ambao si waaminifu.

“Ni kweli wapo watumishi waliokutwa na tuhuma za kuuzia damu wagonjwa, tuhuma dhidi ya mmoja zimethibitika na tayari hayupo kazini, wengine bado tunaendelea na uchunguzi,” alisema.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ni kosa kwa mtumishi yeyote wa afya nchini kumuuzia mgonjwa damu. Damu hutolewa bure na watu huchangia kwa hiari.

Imebainika kuwa chupa ya damu katika hospitali ya Haydom huuzwa kati ya Sh 30,000 hadi Sh 50,000 kutegemea uwezo wa fedha wa mgonjwa au ndugu zake.

Hospitali hiyo ipo katika mji wa Haydom, magharibi mwa Mkoa wa Manyara, umbali wa kilometa 300 kutoka Arusha.

Ilianzishwa mwaka 1955 na wamishionari wa Kilutheri, na kwa sasa inamilikiwa na kuendeshwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mbulu.

Hospitali hiyo inaendeshwa kwa kutegemea fedha kutoka nje, wafadhili wakuu wakiwa ni Serikali ya Norway kupitia Ubalozi wake Tanzania ambayo inachangia zaidi ya asilimia 50 ya bajeti.

Pia Serikali ya Tanzania inachangia kwa kutoa madaktari ambao inawalipa mishahara pamoja na wafadhili binafsi kikiwamo kikundi cha “Marafiki wa Haydom” chenye matawi Norway na Ujerumani.

Pia miradi ya utafiti wa sayansi kuhusu masuala ya tiba ya binadamu inafadhiliwa na Chuo Kikuu cha Virginia cha Marekani na Laerdal cha Norway

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles