31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DAKTARI ‘FEKI’ AKAMATWA MUHIMBILI

NA VERONICA ROMWALD

– DAR ES SALAAM

WALINZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wamemtia mbaroni   Abdallah Athuman, ambaye anatuhumiwa kujifanya daktari   hospitalini hapo.

Tukio hilo lilitokea jana asubuhi   wakati walinzi hao walipokuwa wakifanya doria ndani ya hospitali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Operesheni wa Kampuni ya Ulinzi Nge, Muhimbili, Vitus Kabonge alisema   kijana huyo alikamatwa baada ya kuweka mitego yao.

“Tulipata taarifa zake siku nyingi, tukaanza kufuatilia nyendo zake, tulimkuta akihoji mgonjwa  tukamuita ofisini kwetu ajieleze.

“Tulitaka atupe kitambulisho chake cha kazi na atueleze yupo kitengo gani, hakutupa maelezo, tukamuweka chini ya ulinzi,” alisema.

Akihojiwa na waandishi, Athuman alisema alifika hospitalini hapo kwa nia ya kumsalimia rafiki yake lakini ndipo akashangaa akikamatwa na walinzi hao.

“Nilikuwa pale maeneo ya benki ya damu (Maabara Kuu ya Hospitali), nilikuja kumsalimia rafiki yangu, nikakamatwa.

“Hiki kifaa nilicho nacho shingoni si changu kuna daktari mwanafunzi alikuja akaniachia nimshikie,” alijieleza.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha alisema kijana huyo alifikishwa katika Kituo cha Polisi Salender   hatua za  sheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

“Mtakumbuka miaka mitatu iliyopita kulikuwa na matukio mengi ya namna hii.

“Tuliamua kuweka ulinzi madhubuti kila eneo la kutolea huduma na si rahisi mtu kuwajua walinzi wetu, wakikukamata tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Alisema watu hao wanaojifanya madaktari huwa wanalenga kuwadanganya wateja (wagonjwa) na kuwachukulia fedha wakiahidi kuwasaidia matibabu.

“Kijana huyu ni mfano kwa wengine, walinzi wetu walimkuta akiwahoji wagonjwa, walikwisha kumhisi na kumfuatilia nyendo zake siku nyingi, walimfuata na kumuuliza maswali ya msingi hakuweza kujibu.

“Walimuuliza historia yake ya masomo akadai  amesoma kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1998 hadi 2012 na kidato cha tano na sita mwaka 2013 hadi 14, unaweza kuona anatudanganya kiasi gani,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles