Daktari bingwa: Kuchanganya dawa za kienyeji na kisasa ni hatari

0
1630

Derick Milton, Simiyu

Imeelezwa kuwa kutumia dawa za kienyeji na dawa za kisasa kwa wakati mmoja inasababisha madhara makubwa mwilini kutokana na dawa zote kuwa na sumu tofauti.

Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani na Maradhi kutoka Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Harun Nyagori, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Bariadi kwenye mkutano mkubwa wa Chama cha Wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waandvestista Wasabato (ATAPE) unaoendelea mjini Bariadi.

Katika mkutano huo unaofanyika Mjini Bariadi katika Shule ya Sekondari Kusekwa, Afya ni moja ya huduma zinazotolewa.

“Wagonjwa wengi wanaochanganya dawa hizo wanapata matatizo ya kuharibika kwa figo, kupata matatizo ya moyo, sukari kupanda, pamoja na kuharibika kwa ini.

“Watu lazima watambue kuwa dawa za kisasa asilimia 75 zinatokana na miti shamba na hiyo miti ina sumu ya kuharibu wadudu kwenye mwili, na dawa za kienyeji nazo zina sumu pia, sasa ukichanganya hizo sumu zikakutana ndiyo madhara yanakuwa makubwa,” amesema Profesa Nyagori.

Kutokana na hali hiyo, amesema wanawashauri watu wakiamua kutumia dawa za kisasa wasichanganye na za kienyeji, wakiamua za kienyeji wasichanganye na kisasa, lakini pia wanawashauri wakitaka kutumia za kienyeji wafanye utafiti kwanza kujua kiwango cha sumu kilichomo.

Aidha, amesema kwa muda wa siku mbili tangu mkutano huo umeanza jumla ya watu 269 wamepimwa na 103 kati ya hao wamekutwa na tatizo la presha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here