28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

CUF wajichimbia Z’bar

Pg 1*Wajipanga kutoa mwelekeo April 4

NA KHELEF NASSOR, ZANZIBAR

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Wananchi (CUF), imeanza vikao vyake visiwani Zanzibar chini ya mwenyekiti wake ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CUF, Hamad Masoud Hamad, alisema kikao hicho kitaandaa ajenda kwa ajili ya Baraza Kuu la Uongozi, ambapo pamoja na mambo mengine itaandaa ajenda kuhusu mwelekeo wa chama hicho na hali ya kisiasa Zanzibar.

Alisema kikao hicho kilichoanza jana kitakuwa cha siku mbili ambapo kitafuatiwa na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi kitakachokutana kwa siku mbili kuanzia Aprili 2 hadi 3 mwaka huu.

“Kama unavyojua muda mrefu kama chama hatujakutana kujadili mambo yaliyotokea, sasa kupitia kikao hiki tutazungumzia zaidi hali ya kisiasa Zanzibar pamoja na ajenda kwa ajili ya Baraza Kuu la Uongozi” alisema Hamad.

Alisema hatua ya kutokuwepo katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, chama hicho hakitayumba na badala yake kitakuwa imara zaidi.

Hamadi alisema licha ya hila na vitimbi vilivyofanywa dhidi yao lakini bado wanasimamia msimamo wao wa kutoitambua Serikali iliyopo madarakani kwani haina uhalali kwa mujibu wa sheria.

“Kutokuwepo kwetu Serikalini hakuna maana kuwa CUF itakufa, hilo si kweli, tumepitia masahibu mengi lakini tumeendelea kuimarika, na hili lililofanyika halitoweza kutuyumbisha kamwe,” alisema

Pamoja na hali hiyo CUF imewataka wapenzi na wanachama wao kuendelea kuwa watulivu na kutokubali kuchokozeka na baada ya vikao watatoa tamko ambalo litakuwa dira ya chama hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles