23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CUF waaanza tena na Maalim Seif

Faraja Masinde -Dar es salaam

CHAMA cha Wananchi CUF, kimesema kimeazimia kurejesha ofisi zake zote zilizochukuliwa na chama cha ACT Wazalendo hususan visiwani Zanzibar.

Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaama na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho, Mussa Haji Kombo, ambaye alisema ofisi hizo ni mali ya CUF hivyo ni lazima wazirejeshe.

“Kwa kuwa baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limeazimia kurejesha ofisi  zake zilizoporwa na ACT kupitia kikao chake cha hivi karibuni, sisi viongozi tutazirejesha na tupo tayari kwa lolote na wala hatuna hofu na vitisho vya Maalim Seif (Mshauri wa ACT Sharf Hamad) na wafuasi wake.

“Ikumbukwe ofisi hizi ni za chama chetu, tunaendelea na utaratibu wa kuzirejesha na aSerikali iache kukubali vitisho vya mtu mwenye ubinafsi kupindukia na asiejali umoja na mshikamano wa taifa letu,” alisema Kombo.

Katika hatua nyingine, Kombo alimtuhumu Maalim Seif kuwa ni mbaguzi na mwenye kupandikiza chuki miongoni mwa jamii ya watanzania.

“Unaweza kuona tu kuwa mtu huyu amekuwa chanzo cha kufarakana kwetu kupitia hoja zake mbalimbali zikiwamo za ubara na uzaznzibar hiki ni kielelezo cha uchovu wa fikra zake.

“Hivi kila ahamae chama ataondoka na alichoingia nacho au alichochangia chamani? Kwani Hajji Duni alipohamia Chadema aliondoka na kitu? Au wabunge wa Chadema na CUF walipojiunga na CCM waliondoka na ofisi zao? Hivyo nilazima tutafakari upya jambo hili na tulipinge kwa nguvu zote,” alisema.

Upande wake Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa Chama hicho, Haroub Mohamed Shamis, alisema chama hicho kimechoka kugombanishwa na kufitinishwa kwa maslahi ya mtu mmoja hivyo kimerejea kwenye misingi yake kama ilivyokuwa dhumuni la kuundwa kwake.

“Tumevumilia kwa kipindi kirefu kwa chama kutumiwa na watu wenye maslahi yao akiwamo Maalim Seif Sharif Hamad, amekuwa ni mtu mbinafsi anayeangalia maslahi yake tu.

“Napenda tu niwaambie wanachama wote wa CUF hususani wa Zanzibar kwamba chama chetu sasa kimerejea kwenye misingi yake ya haki na furaha kwa kila mmoja, huku lengo letu kuu likiwa ni kuhakikisha tunashika dola kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles