33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

CRAFT wawekeza Euro milioni 2 uzalishaji chakula

Mwandishi Wetu -Dar es salaam

UZALISHAJI wa chakula katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda, unapaswa kuongezeka ili kutosheleza mahitaji ya wakazi wake ambao idadi yao inaongezeka kwa kiwango cha wastani wa asilimia 3 nchini Tanzania na asilimia 2.5 katika nchi hizo.

Kujifunza kutumia uzalishaji unaoendana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuvuna mazao kisasa na kuchakata mazao ni masuala ya msingi kuongeza uzalishaji na ufanisi wa  mchakato wa sasa wa uzalishaji wa chakula na mifumo ya kukisambaza. 

Ilikufanikisha ongezeko la uzalishaji wa chakula kunahitajika ushirikiano wa wadau mbalimbali kufanya uwekezaji wa pamoja kuanzia wasambazaji, watoa huduma, wafanyabiashara kutoka sekta binafsi, na kuhakikisha kila mmoja katika nafasi yake anatekeleza wajibu wake ipasavyo. 

Mradi mkubwa  wa miaka mitano wa CRAFT, unaojumuisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, umewekeza Euro milioni 2 kwa ajili ya kutoa msaada kwa makampuni 14 ya shughuli za kilimo katika nchi hizi tatu.Uwekezaji  kupitia mradi wa  Climate Resilient Agribusiness for Tomorrow (CRAFT), umelenga makampuni na wakulima wanaojishughulisha na mazao ya alizeti, soya, ufuta, maharagwe, viazi na mtama  na kuongeza myororo wake wa thamani  wa mazao hayo katika nchi hizi tatu. 

Meneja  Mradi wa CRAFT nchini Tanzania, Menno Keizer alisema mradi huu unaoshirikisha sekta binafsi ni mojawapo ya mikakati muhimu inayotambuliwa na mradi ili kufikia matokeo endelevu na kuongeza upatikanaji na uwepo wa chakula kwendana na hali ya hewa iliyopo. Kupitia mpango wa ubunifu kukabiliana na hali ya hewa na kusaidia kufanikisha uwekezaji ((CIIF), mpango huo utasaidia uwekezaji wa msingi wa utendaji ili kujenga nguvu ya makampuni ya kilimo cha biashara kutoka sekta binafsi na watoa huduma ili kufanikisha kuongeza myororo wa thamani kwenye bidhaa zao.

 Hadi sasa kampuni za Tanzania (Nondo Investors Company Limited, Rogimwa Agro Company Limited, Jackma Enterprises Ltd na Mwenge Sunflower Oil Mills) tayari zimesaini mkataba wa makubaliano wenye thamani ya Euro 567,135.

CRAFT imewekeza katika makampuni ambayo yameonekana kuweza kujiendesha kwa mtaji wake, pia kupata fedha kutoka vyanzo vingine (vyanzo vingine ni mikopo kutoka benki) kuhakikisha biashara zake zinazidi kuimarika.

Mradi huu utafanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa lengo la kukuza ubunifu kwenye  kilimo kwendana na hali ya hewa, kuanzia mashambani na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao na kusaidia washirika wake kutoka sekta ya umma kwa kuwajengea mazingira ya kupata mbinu bora za kilimo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles