25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Corona ikiathiri sekta ya anga, Afrika itahitaji uwazi mkubwa kurudisha hali

Na Mwandishi Wetu

Wakati dunia inapambana na kuenea kwa ugonjwa wa corona, ambao hadi sasa umeshasambaa kwenye nchi zipatazo 177 huku watu takribani zaidi 392,000 wakiwa wameathirika na watu zaidi 17,000 wamekufa- sekta ya anga imekuwa miongoni mwa sekta za kwanza zilizoathirika kiuchumi na ugongjwa huo.

Wakati sekta ya anga Afrika yahitaji msaada na hasa lazima tuhakikishe  kuna nafasi ya kubadili hali na kuwa ya uwazi zaidi katika kurudisha hali ilivyokuwa ugonjwa huu utakapo pungua au kwisha kabisa.

Ingawa maambukizi bara la Afrika yanatofautiana kwa kuwa nyuma na maambukizi katika maeneo mengine, mashirika ya ndege katika bara la Afrika yamejikuta yakilazimika kufuta safari zake huku yakipunguza wafanyakazi na kutahadharisha kuwa hali mbaya zaidi itarajiwa siku zijazo.

Tangu mgonjwa wa kwanza kutangazwa, mashirika ya ndege barani Afrika tayari yamepoteza zaidi ya dola za kimarekani 4.4 bilioni kutoka kwenye mapato yao.

Hivi karibuni zaidi, Shirika la ndege la Afrika Kusini limesitisha safari zake za kimataifa baada ya kufunga safari za ndani baada ya hali mbaya ya kifedha kwa mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa Baraza la usafiri na utalii duniani (The World Travel and Tourism Council)  idadi kubwa ya ajira zipatazo milioni moja zinapotea kila siku kutokana na athari za kiuchumi za ugonjwa wa corona.

Wakati huo huo Shirika la kimataifa la Usafiri wa Ndege (IATA) limezitaka serikali zote kuzingatia swala la kusaidia mashirika ya ndege na viwanja vya ndege ambavyo vinapambana kwa kuvipa unafuu wa kodi ikibidi na mikopo pia.

Kwa sababu mashirika ya ndege yatakuja kufanya dunia iinuke na ikimbie tena wakati janga hili la ugonjwa litakapoisha.

Katika kuongezeka kwa uunganishaji wa dunia, tasnia nyingi zinakuwa haraka hutegemea usafiri wa anga, kwa mfano sekta muhimu kama vile utalii itakuwa ni nguzo katika kurejesha mapato ya ndani katika nchi za bara la Afrika.

Hata hivyo, kuna baadhi ya mashirika ya ndege yamekuwa yakitumia mianya ya matatizo na majanga kuweza kujinufaisha yenyewe badala ya kusaidia wateja wake.

Mashirika mengi ya ndege hivi sasa yamekuwa yakifukuza wafanyakazi kwa kisingizio cha ugonjwa wa COVID-19. Hata hivyo kuna taasisi na tume mbalimbali  zimekuwa zikilinda na kutetea maslahi ya wateja, moja ya taasisi hizo ni Tume ya uchunguzi ya Vide Times Live.

Hivi karibuni tume hiyo, imeanza kulifanyia uchunguzi shirika la ndege la Afrika Kusini (SAA) kutokana na tuhuma mbalimbali zinazohusu wafanyakazi, uzabuni , mikataba na ukiukaji wa taratibu nyingi.

Kampuni ingine ambayo ipo katika tuhuma hizo ni Swissport ambayo imekuwa ikidaiwa kufanya maovu mara kwa mara barani Afrika.

Serikali nyingi Kusini mwa Jangwa la Sahara zimekuwa zikipambana na janga la rushwa kwa miaka mingi, huku tawala mpya zinazoingia madarakani zikijaribu kuendeleza mapambano na kuepuka kurudi nyuma.

Sehemu ya matatizo ni matokeo ya uhusiano kati ya Serikali hizo na sekta ya anga kwenye nchi hizo kama vile Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa inategemea utalii, hii ina maana kuwa zinahitaji kuvutia uwekezaji ili sekta ya anga ikue.

Labda kwa mara ya kwanza, mashirika ya ndege na biashara zinatogemea sekta hiyo zitahitaji serikali zaidi kuliko serikali kuhitaji mashirika hayo.

Ugonjwa wa corona utampa changamoto kila mtu, kufanya kazi kwa pamoja kuzuia athari za kiafya na za kiuchumi itafaa zaidi katika kipindi cha wiki kadhaa au miezi ijayo.

Baada ya kuisha kwa janga hili, hata hivyo, jamii itakuwa na nguvu juu ya tasnia ya usafiri wa anga. Ndege, viwanja vya ndege na biashara zinazoendana na sekta hiyo itahitaji msaada kutoka kwa jamii, na tutahitaji uwajibikaji kwa upande mwingine.

Wakati tunapambana kutokomeza COVID-19 kwa pamoja, ni lazima tusonge kwa pamoja kwa uwazi na uwajibikaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles