24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CONTE: SI LAZIMA KUPEANA MKONO

LONDON, England


KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte, amedai kwamba hakukuwa na ulazima wa kupeana mkono na kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, baada ya kikosi chake kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Stamford Bridge, England.

Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata, ndiye aliyeifungia timu yake bao pekee katika ushindi huo, ikiwa ni siku chache tangu wapate kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Roma ya Italia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, baada ya mchezo huo kumalizika, Conte alionekana kumpuuza Mourinho  aliyetaka kumpa mkono na badala yake alienda kushangilia ushindi na mashabiki kabla ya kuhamia kwenye eneo la uwanja ili kuwashukuru wachezaji wake.Mourinho alisimama kwa muda mfupi akisubiri kuona kama Conte angeweza kuona umuhimu wa kupeana mkono kabla ya kuondoka eneo hilo.

“Kupeana mkono si jambo muhimu kama kupata ushindi, hivyo jambo hilo linaweza kuwa muhimu au likawa halina umuhimu lakini jambo kubwa linatakiwa kuonekana ndani ya uwanja,” alisema Conte.

Mourinho alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema: “Conte alikwepa kunipa mkono lakini haina shida kwa kuwa nilifanya hivyo kwa msaidizi wake.”

Umakini ulionekana kuwa mkubwa kwa makocha hao wawili kwa zaidi ya wiki moja kabla ya kuvaana juzi katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Mourinho alionekana kutupiana maneno na mpinzani wake huyo aliyekuwa akilalamika sana juu ya wachezaji wake kuwa na majeraha.Conte ambaye alichukizwa na jambo hilo, alijibu akidai kwamba klabu ya Chelsea kushinda taji la Ligi Kuu England msimu uliopita ulikuwa ni muujiza kwa kuwa alikuwa na wachezaji wengi zaidi ambao walimaliza nafasi ya 10 ilipokuwa chini ya Mourinho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles