24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CONTE AMTAKA MOURINHO KUFUNGA MDOMO

LONDON, ENGLAND


KOCHA wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea, Antonio Conte, amemtaka kocha wa Man United, Jose Mourinho, kufunga mdomo wake na kuacha kuizungumzia Chelsea.

Conte amekuwa na wasiwasi kubwa na kikosi chake kufuatia na idadi kubwa ya wachezaji ambao ni majeruhi msimu huu, hivyo sare ya mabao 3-3 dhidi ya AS Roma kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki hii imezidi kuwaweka kwenye wakati mgumu.

Mourinho ambaye amewahi kuifunsdisha Chelsea mara mbili kwa wakati tofauti, alinukuliwa akisema kuna baadhi ya makocha ambao hupenda kulalamika sana kuhusu wachezaji wao wakiwa majeruhi.

Kauli hiyo ilionekana moja kwa moja kumgusa Conte ambaye amedai ana wakati mgumu wa kutetea taji lake kutokana na baadhi ya nyota wake kuwa majeruhi.

“’Kila mara, Jose Mourinho, amekuwa akizungumzia kile kinachoendelea ndani ya klabu ya Chelsea, hata msimu uliopita alikuwa anaizungumzia Chelsea kila wakati kuliko anavyoizungumzia timu yake.

“Kwa sasa anatakiwa kufunga mdomo wake na kuangalia nini anataka kukifanya katika klabu yake, mwenyewe ana matatizo lakini watu hawana muda huo wa kuzungumzia mambo ambayo hayawahusu,” alisema Conte.

Kwa sasa kikosi cha Chelsea kinawakosa wachezaji wake kama vile kiungo wao, N’Golo Kante, Victor Moses ambao wanasumbuliwa na tatizo la nyama za paja pamoja na Danny Drinkwater, anayesumbuliwa na misuli.

Hata hivyo, katika mchezo dhidi ya AS Roma, nyota wa Chelsea, David Luiz, alipata tatizo la nyama na anaweza kuwa nje ya uwanja katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Watford Jumapili, timu hiyo imepoteza michezo miwili mfululizo ya Ligi Kuu dhidi ya Manchester City na Crystal Palace.

Conte anaamini ana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo bila ya kujali idadi kubwa ya nyota wake kuwa majeruhi kwa kuwa ana kikosi kipana ambacho kinaweza kubadili matokeo muda wowote.

“Unapokuwa na wachezaji wengi ambao ni majeruhi unakuwa na wakati mgumu wa kukiandaa kikosi, lakini sina wasiwasi na mchezo ujao kwa kuwa ninaamini wachezaji waliopo wana uwezo wa kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani,” aliongeza Conte.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles